YAJUE MAZOEA YANAYOWAATHIRI WAFUGAJI WENGI WA KUKU.
Kuna baadhi ya wafugaji huwa wanafuga kwa kutegemea uzoefu
walionao katika ufugaji bila ya kujali kuwa kuna mabadiliko kila siku katika
sekta ya mifugo, wengi wao huwa wanatatua kesi mbalimbali zinazotokea katika
ufugaji kwa kutumia uzoefu hali ambayo inawasababishia kupata hasara kubwa
isiyo ya lazima. Yafuatayo ni baadhi ya mazoea yanayowagharimu wafugaji:-
1. Kuingiza vifaranga bila sahihi.
Wengi wa wafugaji huwa wanaingiza vifaranga pasipo kufuata utaratibu wa kitaalam katika kuandaa banda pamoja na maandalizi ya kupokea vifaranga. Na kama atabahatika kufanya usafi basi atafanya juujuu tu hali ambayo inasababisha banda kuhifadhi vimelea vingi vya magonjwa na kupelekea kuku kuugua na kufa kuanzia wanaingia hadi kufikia kuuzwa, na hatimaye mfugaji hupata hasara kwani hutumia pesa nyingi kwenye madawa kwa kutibu na pesa nyingi kwenye chakula kwa kuchelewa kukua kutokana na kuumwa.

2.
kutibu
kwa dawa ambayo si chaguo sahihi.
Kama inavyofahamika kuwa wafugaji wa kuku wengi
wamebarikiwa kwa kufaham majina mengi ya dawa za kuku, na kwa kutumia uzoefu
walionao huwa wanatibu kuku wao magonjwa mbalimbali bila kupata maelekezo
kutoka kwa Dokta au Mtaalam wa mifugo. Kwa kufanya hivyo hutumia dawa nyingi
tofautitofauti kwa kutibu ugonjwa mmoja bila mafanikio na kupelekea ugonjwa
kuwa sugu na idadi ya vifo kuongezeka siku hadi siku.
3.
Kulisha
kuku bila kufuata utaratibu sahihi.
Kila aina ya kuku wanautaratibu wa ulishwaji
chakula, utaratibu ambao ukikiukwa huwezi kupata matokeo mazuri ya mifugo yako,
ila wafugaji wengi huwa wanalisha kwa utaratibu usio sahihi ambao wao wanadhani
kwamba ndio wataongeza uzalishaji wa mayai au watakuwa haraka kwa upande wa
kuku wa nyama, na kuna wengine wanadiriki kutumia chakula aina moja mwanzo
mwisho, yaan anaweza kutumia chakula cha vifaranga wa nyama (SUPER STARTER)
kuanzia mwanzo hadi anauza kuku bila kufaham kwamba kila aina ya chakula ina
kazi yake katika kila hatua ya umri. Lakini pia bila kujali kwamba analisha kwa
gharama kubwa hali ambayo itampunguzia faida.
USHAURI: Sio kila mfugaji mzoefu anaweza kuwa
Daktari, ila kila Daktari anaweza kuwa mzoefu.
YAJUE MAZOEA YANAYOWAATHIRI WAFUGAJI WENGI WA KUKU.
Reviewed by BENSON
on
November 05, 2017
Rating:
No comments