JISNI YA KUFANYA MATUNZO YA KUKU WANAOTAGA.
Hapa tunaangalia majogoo na mitetea yenye umri wa kuanzia
miezi minne na kuendelea. Matunzo mengi wanayopewa
ni sawa na ya kuku wanaokua (tafadhali rejea kwenye somo la matunzo ya kuku
wanaokua).
Matunzo mengine ya ziada:-
1. Watenge majogoo na matetea kwa idadi inayofaa.
Kama unafuga huria, jogoo mmoja kwa mitetea 6.
Kama unafuga kwenye vyumba, jogoo mmoja kwa mitetea 4-5.
2. Wape chakula cha ‘ layers’ chenye virutubisho vya kutosha.
3. Endelea kuchanja Newcastle kila baada ya wiki 10.
4. Endelea kuwapa dawa ya minyoo kila baada ya wiki 10.
5. Walishe majani na mboga mboga kwa wingi, ili mayai watakayotaga yawe na kiini cha njano.
6. Kuwa makini sana na sehemu ya kifua na eneo la chini la mitetea, ambapo ndipo mayai yanapohifadhiwa kwa ndani. Kuku akigongwa au akijigonga eneo hilo, yai linaweza kupasuka kwa ndani, na tetea huyo atanyong'onyea, na baada ya siku kadhaa atakufa.
7. Okota mayai mara nyingi iwezekanavyo, ili kuzuia kuku kula mayai au wasiyavunje au kuyawekea ufa.
8. Kuku wanapoanza kutaga nunua daftari ya kutunza kumbukumbu za mayai yanayotagwa kila siku. Hii itakusaidia kujua siku wanapopunguza kutaga, ili kutafuta chanzo, na kama ni ugonjwa, watibiwe haraka.
Kila la kheri katika ufugaji wako, na endelea kuwa pamoja nasi katika masomo mengine ya ufugaji wa kuku.
JISNI YA KUFANYA MATUNZO YA KUKU WANAOTAGA.
Reviewed by BENSON
on
November 02, 2017
Rating:
No comments