SIFA ZA BANDA BORA LA KUIGUGIA KUKU.
Wakati unataka kuanza kufuga kuku lipo jambo la
muhimu ambalo ni muhimu sana kuliweza kulifikiria, na jambo hilo si jingine
bali ni banda kwa ajili ya kufugia kuku. Zifuatazo ni sehem za banda bora la
kuku kulingana na aina ya kuku:-
1. Sehem za kutagia
(kama ni kuku wa mayai au wa kienyeji).
Katika banda bora la kuku wanaotarajiwa kutaga
inapaswa kuwepo na sehem za kutagia zijulikanazo kwa jina la viota. Viota
vinaweza kutengenezwa kwa mtindo wa kuku mmoja mmoja au ushirika.
2. Sehem ya kutembelea.
Ni ukumbi mkubwa kulingana na idadi ya kuku, ambao
ndani yake kunakuwa na vyombo vya maji na chakula, pamoja na kuku wenyewe.
3. Sakafu
Zipo aina mbalimbali za sakafu kama ifuatavyo:-
·
Sakafu
ya saruji; Ni vema
zaidi ukajenga sakafu ya saruji kisha ukaweka maranda juu yake ili kuzuia ubaridi unaotoka sakafuni, na vilevile
kupata wepesi wakati wa kufanya usafi.
·
Sakafu
ya udongo au mawe;Jaza
udongo wa mfinyanzi au mawe kisha siliba vizuri acha pakauke mwisho weka Maranda
kwa wingi.
·
Sakafu
ya chaga; Banda hujengwa kisha huwekwa chaga umbali wa futi
mbili kutoka chini, chaga inaweza ikawa ya banzi, "chicken wire" au
fito ili kuruhusu kinyesi cha kuku kudondoka choini.
4. Ukuta
Unaweza kujenga ukuta kwa kutumia nguzo, pamoja na
mabanzi au fito kisha kuzibwa vizuri na kuacha sehemu kubwa kwa ajili ya
madirisha. Pia unaweza kutumia tofali za kuchoma, saruji au tofali za udongo
kwa kujengea na kuacha sehem kubwa kwa ajili ya madirisha.
5. Paa
Vifaa vya kuezekea
vinaweza kuwa ni vigae, nyasi, makuti au bati.
Kwa heshima na taadhima napenda kutumia fursa hii
kukusalimia wewe mdau wa mifugo na ambaye si mdau wa mifugo lakini
unapenda kufuatilia mafunzo yetu.
Pia napenda kuwakaribisha katika darasa letu la
ufugaji, tutakuwa tunawaletea
mada mbalimbali zinazohusu masuala mazima ya
ufugaji.
Lengo kuu la darasa letu la ufugaji ni
kumfanya mfugaji afuge kwa......
kufuata kanuni za ufugaji bora ili
ufugaji wake uwe ni wenye tija na kumpatia faida kwa ujumla.
Malengo mengine kama yafuatayo:
- Kumfanya mfugaji aboreshe maisha yake kupitia
ufugaji mifugo yake
- Kuboresha afya za watumia mazao ya mifugo kama
vile, Nyama, Mayai, na Maziwa kwa kuwa watatumia mazao ya mifugo kwa
kanuni bora za ufugaji.
- Kuongeza upatikanaji wa ajira kwa
vijana, watu wazima na wazee kwa ujumla kupitia ufugaji mdogo wa kati na
mkubwa.
- kuongeza matumizi sahihi ya nguvu kazi
na rasilimali watu kupitia ufugaji.
Hivyo basi ukiwa kama mdau wa mifugo au si
mdau lakini unapenda kufatilia darasa letu, tunakukaribisha tena na
tena katika kufatilia mfululizo wa mada mbalimbali katika darasa letu
tunasema karibu sana
SIFA ZA BANDA BORA LA KUIGUGIA KUKU.
Reviewed by BENSON
on
November 03, 2017
Rating:
No comments