JINSI YA KUTENGENEZA BUSTANI NDOGO NYUMBANI

Kuna njia mbali mbali waweza kuepuka kutumia mboga mboga zinazolimwa usikokujua na kuepuka kujiingiza katika afya mbaya kwa matumizi ya kemikali za kuulia wadudu na magonjwa zinazotumika katika ukuzaji wa mboga mboga.

Aina za bustani

1. Unaweza tumia makopo amabayo mara nyingi hutumika kupanda maua kando kando ya nyumba
2. Unaweza tumia gunia la sandarusi kubwa..
3. Unaweza tengeneza key hole garden ( bustani ya tundu la Ufunguo)

Bustani Ya Makopo/Ndoo 

Vifaa
Udongo, makopo/ndoo, mchanga/Pumba za mpunga (Rice husk), Mbole ya samadi iliooza vizuri.
Udongo - Kwa ajili ya kuwezesha mmea kusimama, pia kupatia virutubisho mmea
Mchanga/Rice husk - Kusaidia mizizi kupita kwa urahisi, pia kuweka mazingira mazuri ya hewa na maji katika udongo yaani mzunguko wa maji na hewa. 
Mbolea ya samadi - Kutoa virutubisho kwa mmea
Hatua za utengenezaji.
- Changanya udongo wako na mchanga/rice husk pamoja na mbole katika uwiano wa 5:2:1.
   5 udongo, 2 samadi, 1 Mchanga/rice husk
- Toboa makopo yako kwa chini ili kuzuia maji kubaki kwa wingi kwenye kupo na weka pamba kwenye matundu uliotoboa.
- Weka udongo uliochanganywa vizur kwenye makapo/ndoo. Hapo utakuwa tayar kupanda mbegu zako ama mche wa mboga aina yoyote.
 - Kuepuka uchafuzi wa mazingira kwa maji yanayo toka kwenye makopo endapo makopo hayo yapo kwene simenti, weka makopo/ndoo hayo juu sahani/besen
Uangalizi.
- Mwagilia mboga yako mara tu baada ya kupanda na kuendelea ikitegemeana ni aina gani ya mboga.
- Unapoona magonjwa hasa fangasi wa ukungu na wadudu wa mboga unaweza tumia dawa zisizo za kemikali za viwandani kama vile  majani ya pilipili kichaa, mwarobaini na tumbaku.
- Mboga kama sukuma wiki waweza vuna mara kwa mara, kazi yako ni kumwagilia tu.
- unatakiwa kubadilisha udongo wako kwa muda mfano. baada ya mavuno 2 ili kuakikisha mboga zako zina pata virutubisho ya kutosha.. ( Hii inategemeana ni aina gani ya mboga)
Faidi
- Inapunguza utumiaji wa kemikali za viwandani
- Gharama za uhitaji wa mboga za majani.
SEHEMU YA PILI 

BUSTANI YA GUNIA

Vifaa
Udongo, Kokoto (mawe madogo madogo), Gunia, mchanga/Pumba za mpunga (Rice husk), Mbole ya samadi iliooza vizuri, mti/mbao na kopo dogo (sadolini).
Udongo - Kwa ajili ya kuwezesha mmea kusimama, pia kupatia virutubisho mmea
Mchanga/Rice husk - Kusaidia mizizi kupita kwa urahisi, pia kuweka mazingira mazuri ya hewa na maji katika udongo yaani mzunguko wa maji na hewa. 
Kokoto  - Kusadia maji kupita ndani ya gunia toka juu hadi chini
Mbolea ya samadi - Kutoa virutubisho kwa mmea
mti/Mbao  - Kusaidia gunia lako kusimama vyema/ imara
Hatua za utengenezaji.
  (i)   Changanya udongo wako na mchanga/rice husk pamoja na mbole katika uwiano wa 5:2:1.
         5 udongo, 2 samadi, 1 Mchanga/rice husk.
(ii)    Toboa kopo lako na ondoa kitako ili kuweka uwazi pande zote mbili (juu na chini)
(iii)  Weka mti/ubao katikati ya gunia ukiuchimbia ardhini kisha weka kopo lako katikati ya mti/mbao hiyo na lijaze kokoto 
(iv)  Weka udongo uliochanganywa vizur kwenye gunia lako ukilizunguka kopo lenye kokoto hadi kufikia kimo cha kopo. Baada ya hapo ondoa kopo na hakikisha kokoto zinabaki zikizungukwa na udongo.
(v)  Weka kopo juu ya kokoto zilizozungukwa na udongo kisha, lijaze kopo hilo na kokoto, rudia kujaza udongo ukilizunguka kopo hadi kimo cha kopo hilo. Endelea kufanya hivyo (kama hapo juu) hadi pale gunia lako litakapokuwa limejaa.
 (vi) Toboa gunia kwa kuweka matundu kuzunguka gunia kwa ajili ya kupandia katika umbali sawa (inategemea na aina ya mboga)
 (vii) Hapo utakuwa tayari kupanda mbegu zako ama mche wa mboga aina yoyote juu na pembeni ya gunia lako
Mboga aina ya letuce (Lactuca sativa)
 Mboga aina ya sukumawiki (Brassica carinata) zikiwa zimepandwa kwenye gunia
Uangalizi.
- Mwagilia mboga yako mara baada tu ya kupanda na kuendelea ikitegemeana ni aina gani ya mboga.
- Unapoona magonjwa hasa fangasi wa ukungu na wadudu wa mboga unaweza tumia dawa zisizo za kikemikali za viwandani kama vile  majani ya pilipili kichaa, mwarobaini na tumbaku.
- Mboga kama sukuma wiki waweza vuna mara kwa mara, kazi yako ni kumwagilia tu.
- unatakiwa kubadilisha udongo wako kwa muda mfano. baada ya mavuno 2 ili kuakikisha mboga zako zina pata virutubisho ya kutosha.. ( Hii inategemeana ni aina gani ya mboga)
Muhimu: Ukitumia miche kwa siku tatu/mbili za mwanzo usije ogopa kuona miche yako imelala endelea kuimwagilia itasimama tu. Pia katika umwagiliaji hakikisha unamwaga maji katika kati ya guni pale kulipo na kokoto ili kuhakikisha maji yanasamba ndani ya gunia hadi chini.
Faidi
- Inapunguza utumiaji wa kemikali za viwandani
- Gharama za uhitaji wa mboga za majani.
- inatumia nafasi ndogo na kutoa kiasi kikubwa cha  mboga mboga.
 

JINSI YA KUTENGENEZA BUSTANI NDOGO NYUMBANI JINSI YA KUTENGENEZA BUSTANI NDOGO NYUMBANI Reviewed by BENSON on November 21, 2017 Rating: 5

No comments