UFAHAMU UGONJWA MNYAUKO FUSARI KATIKA KILIMO CHA KAHAWA - COFFEE FUSARIUM


Ugonjwa huu husababishwa na vimelea vya fusari. Hushambulia mashina, machipukizi na hata punje. Ugonjwa wa mnyauko fusari unashamiri kwenye mashamba ambayo hayatunzwi vizuri inavyopasa. Viini vya ugonjwa huu vinauwezo mdogo sana wa kushambulia
mkahawa wenye afya nzuri, ukiona shamba limeshambuliwa na uonjwa huu jua moja kwa moja kwamba shamba hilo halitunzwi vizuri kwa kufuata kanuni za kilimo bora.

DALILI KUU:
Machipukizi yaliyoshambuliwa na ugonjwa huu hunyauka, na majani hubadilika na kuwa na rangi ya kahawia. Matawi na mashina yakishambuliwa hunyauka na kufa. Ukitaka kuthibitisha dalili za fusari kata shina utaona miviringo ya kahawia. (Brown ring)

JINSI YA KUZUIA
• Palizi ni muhimu kwenye shamba.
• Ukataji sahihi wa matawi.
• Matumizi ya mbolea kwa kiwango kinachoshauriwa.
• Ng’oa na choma moto mikahawa iliyokufa.
• Iwapo ni matawi yanayoonyesha dalili za ugonjwa matawi hayo yakatwe na kuchomwa moto.

NB: Miche mingine ya kahawa isipandikizwe sehemu ilikong’olewa
mikahawa yenye ugonjwa kabla ya miezi sita.
UFAHAMU UGONJWA MNYAUKO FUSARI KATIKA KILIMO CHA KAHAWA - COFFEE FUSARIUM UFAHAMU UGONJWA MNYAUKO FUSARI KATIKA KILIMO CHA KAHAWA - COFFEE FUSARIUM Reviewed by BENSON on October 19, 2017 Rating: 5

No comments