JIFUNZE KANUNI BORA KILIMO CHA BAMIA
Jinsi ya kupanda bamia.
Mambo muhimu ya kuzingatia katika kilimo cha bamia.
Hakikisha ;
- Unatumia mbegu bora
- Panda kwa nafasi
- Mwagilia maji ya kutosha
- kulingana na hali ya hewa
- Palilia shamba vizuri
- Dhibiti magonjwa na wadudu waharibifu kwa wakati
- Vuna kwa wakati unaotakiwa
Mbegu mbili zipandwe kwenye shimo moja. Nafasi ya upandaji iwe ni sentimita 30 toka shimo hadi shimo na sentimita 50 toka mstari hadi mstari. Kwa aina ya bamia zinazorefuka sana iwe sentimita 40 kati ya shimo na shimo na sentimeta 70 kati ya mstari na mstari.
Kama unyevu wa ardhi hautoshi, inapendekezwa kutumia mojawapo ya njia za kumwagilia maji bustanini kulingana na hali ya hewa ya eneo husika.
Palizi
Hakikisha shamba ni safi wakati wote kwa kuondoa magugu mara tu unapoona yamejitokeza ili kuongeza uzaaji wa bamia.
Wadudu waharibifu
Wadudu wanaoshambulia zao hili la bamia kama vile kimamba, funza wa vitumba na utitiri mwekundu. Dhibiti wadudu hawa kwa kufuata njia zinazopendekezwa na wataalamu wa kilimo Kwenye eneo lako.
Bamia hushambuliwa na magonjwa kama ukungu, ubwiri poda na kunyauka huathiri zao la bamia hivyo ni vyema kuzuia kwa kufuata mzunguko wa mazao na kutumia dawa kulingana na ushauri wa wataalamu wa kilimo eneo ulipo.
Bamia huvunwa kabla ya kukomaa yaani zikiwa bado changa.
Unashauriwa kutumia kisu kuvunia na uhakikishe unavuna bamia na kikonyo chake ili kupunguza kuharibika kwa bamia Kiasi cha kilo 8000 zaweza kupatikana katika ekari moja iwapo zitatunzwa vizuri.
Mpaka hapo hatuna la ziada. Asante kwa kuwa sehemu yetu.
JIFUNZE KANUNI BORA KILIMO CHA BAMIA
Reviewed by BENSON
on
October 13, 2017
Rating:
No comments