KILIMO BORA CHA STRAWBERRY
Zao hili hustawi katika joto la wastani, na hukua kwa haraka zaidi na
uzalishaji kuongezeka linapolimwa kisasa, hasa katika nyumba maalumu ya
kuzalishia mimea yaani green house. Katika Tanzania zao hili linakuwa vizuri
mikoa ya Morogoro na IringaZao hili hukua vizuri katika mwinuko wa mita 1,500
kutoka usawa wa bahari.
Endapo unahitaji kuzalisha strawberry katika maeneo ya bondeni
itakulazimu kuwa na maji kwa wingi kwa ajili ya umwagiliaji wa mara kwa mara.
Strawberry inaweza kustawi vizuri kwenye udongo tifutifu wenye rutuba. Zao hili
haliwezi kustahimili ukuaji kwenye udongo wenye chachu nyingi, hasa chokaa
kwani mizizi yake huoza kwa urahisi.
KUPANDA
Ili kuwa na mazao bora ambayo yatakuwezesha kupata soko la
uhakika, bila vipingamizi, inashauriwa kuzalisha kwenye nyumba maalumu ya
kuzalishia mazao (green house). Katika kuzalisha strawberry baada ya kujenga
green house andaa mabomba ya plastiki ambayo yatawezesha kutoboa matundu kwa
urahisi Matundu katika bomba hilo yawe na umbali wa inchi 1.
1. Ni vyema matundu
hayo yakawa zigzag, ili kuruhusu mimea utakayopanda kukua vizuri bila kuwekeana
kivuli.
2.
Tandika karatasi la
nailoni sakafuni ili kuwezesha maji utakayotumia kunyeshea kurudi kwenye bwawa
au sehemu ya kuhifadhia.
3.
Ning’iniza mabomba hayo
kwa kutumia waya.
4.
Jaza kokote, yenye
mapande makubwa kiasi.
5.
Panda miche kwenye kila tundu kwa uangalifu ili mizizi isikatwe
na kokoto zinazoshikilia mmea. Kumwagilia Mimea ya strawberry inahitaji maji
kwa kiasi kikubwa sana. Hii inamaanisha kuwa unahitaji kuwa na mfumo mzuri wa
umwagiliaji kabla ya kuanza kilimo cha zao hili.
6.
Unapaswa kumwagilia mara nne kwa siku, kila baada ya saa nne
unapaswa kumwagilia kwa robo saa. Hii itawezesha mimea yote kupata maji ya
kutosha. Endapo strawberry haitapata maji ya kutosha, uzalishaji wake pia
utakuwa ni hafifu sana, kwani maua ya Strawberry inapooteshwa kwenye greenhouse
hutoa mavuno mengi na yenye ubora yatachanua ipasavyo na hata matunda kukomaa
inakuwa ni shida.
Mbolea
Uzalishaji wa kisasa wa strawberry, unaambatana na ufugaji wa
samaki kwenye bwawa ndani ya green house. Mbinu hii husaidia mimea kupata
mbolea inayotokana na chakula wanacholishwa samaki kwenye bwawa, kwani maji
yanayofugia samaki ndiyo hayo yanayotumika katika mzunguko wa umwagiliaji. Hii
inamaanisha kuwa hakuna mbolea nyingine inayohitajika kwa ajili ya strawberry.
Wadudu na magonjwa Endapo strawberry inazalishwa kwenye nyumba maalumu ya
mimea, hakuna magonjwa wala wadudu wanaoishambulia.
Uzalishaji wa
green house.
Ikiwa mkulima anazalisha strawberry kwenye eneo la wazi,
strawberry inaweza kushambuliwa na magonjwa ya ukungu, pamoja na magonjwa
yanayosababishwa na virusi.
Dawa.
Endapo strawberry itashambuliwa na magonjwa ya ukungu na virusi,
nyunyizia dawa za asili kama vile pareto na mwarobaini, na baada ya muda
kutakuwa na matokeo mazuri.
Kuvuna.
Zao la strawberry, huzaliana na kukomaa kwa haraka sana. Unaweza kuanza kuvuna
strawberry baada ya mwezi mmoja tangu kupandwa. Kila wiki strawberry inakuwa na
matunda mapya, na kila tunda likishatokeza huiva kwa haraka, hivyo uvunaji wake
ni wa mfululizo. Ikishafikia hatua hiyo tegemea kuwa na wiki 2 hadi 3 za kuvuna
mfululizo.
Kwa kuwa matunda ya strawberry ni laini, epuka kushika tunda
wakati wa uvunaji ili lisiharibike. Shika kikonyo cha tunda ili kuvuna kwa
usalama. Usiache matunda yaliyoiva shambani kwa muda mrefu kwani yanaweza
kusababisha mimea kuoza.
Pia yatapoteza ladha na virutubisho halisi vinavyotakiwa.
Virutubisho Strawberry ina kiasi kikubwa cha virutubisho hasa vitamin B, C, K,
na E . Pia yana wingi wa madini ya chumvi. Matunda haya husaidia kuchangamsha
mwili na yana kiasi kidogo cha kalori.
Matumizi
Matunda ya strawberry yana matumizi mbalimbali kulingana na
uhitaji wa mtumiaji, jamii na maeneo. Miongoni mwa matumizi hayo ni pamoja na:
1. Kuliwa kama tunda.
2.
Kutia ladha katika aina
mbalimbali za vyakula. •
3.
Kuweka rangi, harufu na nakshi katika vipodozi. •
4.
Kutengeneza marashi n.k.
Soko:
Soko
zuri kulingana na ubora wake. Kwa sasa gramu 500 za strawberry zinauzwa kati ya
shilingi 5,000/= hadi 10,000/= za kitanzania.
KILIMO BORA CHA STRAWBERRY
Reviewed by BENSON
on
November 07, 2017
Rating:
No comments