MBINU BORA ZA KULEA VIFARANGA VYA KUKU
Kuna
vitu vya msingi katika uleaji wa vifaranga vya kuku. Uleaji huu hutofautiana
kati ya vifaranga wa kuku wa mayai, kienyeji na kuku wa nyama katika chakula na
chanjo kwa ujumla
MATAYARISHO
·
Banda
liwe imara kuepuka wizi na wanyama wasumbufu kama ngoja, paka, mbwa, mwewe, na
kecheche.
·
Banda
liwe linaweza kuingiza hewa ya kutosha na kavu isiyo na unyevunyevu.
·
kabla
ya kuingiza safisha banda nje na ndani kwa kutumia dawa ya kuua vijidudu vya
magonjwa. Paka chokaa kuta za ndani na hakikisha banda haliwi na joto Kali,
baridi kuingiza, mbua na upepo mkali.
·
Tayarisha
chakula bora.
·
vifaa
vya kulishia na kunyweshea maji.
·
Tandiko
safi, kama vile maranda, pumba za mchele.
·
Dawa
KABLA YA KUFIKA VIFARANGA
Banda
liwe tupiu kwa wiki moja baada ya kusafisha kwa dawa. Vifaranga utakaopewa
watoke kwenye mzalisha mwenye historian nzuri.
·
Usichanganye
vifaranga wa sehemu tofauti.
·
Vifaranga
huweza kuathirika haraka na mazingira hivyo yafaa kuwa na uangalifu wa hewa,
mwanga na joto.
·
Vifaa
vya mwanga na joto ni muhimu na lazima katika kulea vifaranga.
·
Tangazi
za msuara kwa kutumia hard board yenye urefu wa sentimita 60 na katikati weka
balbu au Niko la mkaa na taa ya mafuta; Kwisha mwanga wa kutosha ili vifaranga
waone chakula na maji.
·
weka chokaa halafu maranda na tandiko chilk
paper au magazeti juu. ya maranda.
·
Masaa
matano kabla ya kufika vifaranga washa taa za joto au jiko la mkaa kwa ajili ya
joto kwa vifaranga, joto liwe na nyuzi joto 32-35.
·
Hakikisha
joto loinakuwa la wastani.
Wiki ya kwanza - 35°c
Wiki ya pili - 32°c
Wiki ya tatu - 29°c
Wiki ya nne - 26°c
Wiki ya kwanza - 35°c
Wiki ya pili - 32°c
Wiki ya tatu - 29°c
Wiki ya nne - 26°c
MUHIMU
Iwapo
vifaranga wanatoka mbali na wamechoka wape glucose au sukaei kidogo kwenye maji
( kijiko cha chakula kwa kila Lita tank za maji).
KUPOKEA VIFARANGA
Watoe
vifaranga kwenye maboksi kwa haraka na kuwaingiza kwenye mduara au hard board
uliyoiandaa na hakikisha unayo hesabi kamili.
·
vifaranga
wore kwenye maji ya glucose watoe nauwanyweshe wale wore ambao hawakunywa maji.
·
Baada
ya masaa mawili weka chakula kwenye vyombo hakikisha kuna mwanga saa 24 na joto
la kutosha.
MBINU BORA ZA KULEA VIFARANGA VYA KUKU
Reviewed by BENSON
on
March 02, 2018
Rating:
No comments