KANUNI ZA KUANDAA KITALU CHA MBOGAMBOGA.
·
Tengeneza tuta la kubwa wa 1m x 2m
(ama urefu unaoona wewe kuwa unakufaaa ila tu upana ubaki kuwa 1mita) . Urefu
na idadi ya matuta hutegemea kiasi cha
mbegu. Kiasi cha mbegu kwa hectare moja ni kilo 6 au 2 kg kwa eka.
mbegu. Kiasi cha mbegu kwa hectare moja ni kilo 6 au 2 kg kwa eka.
·
Weka samadi iliyooza vizuri kiasi
cha debe moja au mchanganyiko wa mbolea ya TSP na CAN (200gm) kwa uwiano wa 1:1
kwenye tuta changanya vizuri na udongo.
·
Sia mbegu kwenye mistari kwa nafasi
ya 1 sm x 20 sm. Tawanya mbegu vizuri wakati wa kusia ili miche isisongamane.
·
Funika mbegu na weka matandazo ya
nyasi kavu juu ya tuta na mwagiliwa maji. Udongo unatakiwa kuwa na unyevu kiasi
mpaka mbegu ziote.
·
Nyasi ziondolewe mara tu mbegu
zikiota .
·
Miche itunzwe vizuri na kitalu kiwe
katika hali ya usafi.
·
Miche imwagiliwe maji mpaka ifikie
umri wa kupandikiza shambani.
·
Sehemu ya kitalu iwe wazi, mbali na
kivuli na kiwe karibu na chanzo cha maji.
KUMBUKA:siku za ukaaji wa mbegu kitaruni inategemeana na aina ya
mbegu ama zao.
KANUNI ZA KUANDAA KITALU CHA MBOGAMBOGA.
Reviewed by BENSON
on
March 16, 2018
Rating:
No comments