TENGENEZA CHAKULA CHA KUKU, NGURUWE NA NG`OMBE KWA KUTUMIA TEKNOLOJIA YA HYDROPONICS
Tumerahisisha
zaidi maelezo na kuifanya iakisi mazingira harisi ya mfugaji wa kitanzania
Hydroponic
ni nini?
Ni
mbinu ya kukuza mimea kwa kutumia mchanganyiko wa virutubisho vya madini katika
maji bila kutumia udongo. Mchakato huu huchukua siku 6 hadi tisa kukamilika.
Kilo
moja ya mbegu huzalisha wastani wa kilo 6 hadi kumi za majani na mizizi.
Faida
za Teknolojia hii
i.
Malisho huzalishwa ndani ya muda mfupi katika eneo dogo.mfano eneo la 4X3 mita
huweza kutoa malisho sawa na ekari 2.
ii.
Chakula hiki hulika chote kwa mifugo. Wanakula najani yote pamoja na mizizi.
Hakuna upotevu wa chakula.
iii.
Mahitaji ya maji ni madogo na maji yanaweza kutumika tena na tena.
iv.
Gharama za uendeshaji wake ni mdogo; hakuna kuandaa ardhi, palizi na gharama za
uvunaji.
v.
Uwezekano mdogo sana wa wadudu ama magonjwa kushambulia.
Faida
katika ulishaji
i.
Chakula hiki ni laini hivyo mmengényo wake katika mifugo ni mkubwa hivyo sehemu
kubwa hutumika katika mwili wa mifugo na uzalishaji.
ii.
Mazao ya mifugo uboreka zaidi na kuendana na mahtaji ya soko. Mfano:
ü mayai ya kuku huwa na kiini cha
njano zaidi wanapokula majani.
ü Maziwa huwa na uwiano mzuri wa
Omega 3 na Omega 6 amino acid ambazo hujenga afya imara ya mlaji.
iii.
Hupunguza gharama za chakula na hivyo kuongeza faida.
iv.
Virutubisho vingi hasa vitamin ambazo huchangia afya ya mifugo kuimalika.
v.
Kinapolishwa kwa mchanganyiko na vyakula vingine kwa uwiano tutakaoutoa hapo
mbele, uzalishaji na ukuaji wa mifugo huwa mzuri zaidi.
Vifaa
mihimu
Ø Sehemu/chumba cha kukuzia.
Ø Nguzo na fito za kutengeneza
chanja kwa ajili ya kupanga trei.
Ø
Trei za plastiki/aluminiamu.
Ø
Dawa yenye Chlorine (kama Waterguard) ama JIK kuua vijidudu katika maji na
mbegu.
Ø Virutubisho (nutrients): wengine
hutumia buster za mazao (hakikisha haina madhara kwa mifugo).
Ø
Pump (sprayer) kunyunyiza maji.
Ø Mbegu.
Mbegu
zinazoweza kutumika
Shayiri,
mahindi, ngano, mtama na nafaka nyingine nyingi.
SEHEMU
YA PILI
UZALISHAJI
WA MALISHO KWA TEKNOLOJIA YA HYDROPONIC
SEHEMU
YA PILI
HATUA
KWA HATUA KATIKA KUZALISHA HYDROPONIC
Kwa
kufuata hatua hizi unaweza kuzalisha malisho yako mwenyewe nyumbani.
1.
Chagua mbegu ambazo hazijaanza kuchipua, na hazina kemikali ama dawa ya aina
yoyote.
2.
Loweka mbegu katika mchanganyiko wa maji na Chlorine kwa masaa mawili kuepusha
kuvu/uvundo ama vimelea vya magonjwa kumea na kukua.
3.
Zitoe mbegu kwenye maji, zioshe kisha ziloweke kwenye maji safi kwa masaa 24
kuwezesha mbegu kufyonza maji vema.
4.
Katika kupanda mbegu, pima kilo mbili za mbegu kwa kila trei yenye urefu wa Cm
80 kwa upana wa Cm 40.
5.
Sambaza mbegu kwenye trei kwa usawa, (zisizidi Cm 3 kimo) ili kuwe na nafasi ya
kutosha kwa kila mbegu kuchipua (kuota).
6.
Hakikisha trei zina matundu kwenye kitako (chini) ambayo yamesambaa kwa usawa
kuwezesha maji ya ziada kutoka.
7.
Hamishia trei kwenye chanja ulizotengeneza. Mbegu zitaanza kuota katika hatua
hii. Fanya hii ni siku ya kwanza.
8.
Nyunyizia maji (kwa pampu) toka siku ya kwanza hadi ya sita, kwa mara nne
katika kila masaa 24.
ZINGATIA.
Mbegu
zenye dawa au sumu yoyote ni hatari kwa wanyama. zinaweza kuwadhoofisha ama
kuwaua. hakikisha hautumii mbegu zenye dawa.
Jinsi
ya kulisha
Kuku:
kwa kuku 100 wanaotaga (layer) wape kilo 8 za hydroponics na waongezee
kilo 4 za chakula cha ‘layer’ (layer mash) kwa siku.
Nguruwe:
katika unenepeshaji wape kilo 2 za hydroponics na 1.5 za chakula kikavu
(nafaka) kwa nguruwe mmoja kwa siku.
Ngómbe,
mbuzi: wanaweza kutegemea majani haya tu na kuwa na uzalishaji mzuri bila
nyongeza ya mchanganyiko wa nafaka. Kama uzalishaji wa maziwa ni mkubwa sana
(zaidi ya lita 12 kwa siku) ni vema kuwaongezea nafaka.
Sungura:
wanaweza kutegemea majani haya tu lakini ni vema kuwapa nyongeza ya
mchanganyiko wa nafaka (angalau kwa uwiano wa 50%).
TENGENEZA CHAKULA CHA KUKU, NGURUWE NA NG`OMBE KWA KUTUMIA TEKNOLOJIA YA HYDROPONICS
Reviewed by BENSON
on
February 03, 2018
Rating:
No comments