CANNIBALISM KWA KUKU NINI?
"Cannibalism,"
Kudonoana kwa kuku ni tatizo linalo wa sumbua wengi, ni moja ya athari ya lishe
duni. Ni kisema lishe duni na maanisha chakula wanacho kula kukosa vurutubisho
muhimu vya madini au kuku kutokula chakula cha kutosha.
#Hizi ni moja ya sababu zinazo pelekea kuku kudonoana.
1.Kuku kukaa wengi kwenye eneo dogo
2. Tabia yao
3.Ubaguzi wa rangi
Hii Mara nyingi hutokea kwa kuku weusi ukiwachanganya na kuku mweupe au
rangi ingine tofauti, kuku weusi Mara nyingi huwa ni wakali sana Kwahiyo ukiona
kuku bandani kwako kadonolewa chunguza kwa makini chanzo ninini! Kama ni
ubaguzi wa rangi unaweza watenga hao weusi.
4. Kuku kutokupata chakula cha kutosha
5.Upungufu wa madini ( protini)
6. Kukosa kitu walicho kizoea au kuboreka
Kwa mfano kuku ukiwazoesha kuwa changanyia Damu kwenye chakula , siku
utakapo punguza kipimo au kuacha kabisa kuwa changanyia damu ambayo
umewazoesha kuwa changanyia lazima watadonoana.
Kuku ukiwa zoesha kuwa fungia mchicha hasa wale kuanzia mwezi mmoja hadi
wa miezi 4 siku utakapo acha kuwafungia mchicha inaweza sababisha
wakadonoana.
Kuku hupenda kuparuaparua na kuzunguka zunguka. Wakikosa nafasi na vitu vya
kudonoa donoa huanza kudonoana wenyewe kwa wenyewe.
7. Mwanga mkali
8. Msongo
Banda lenye joto sana na lisilo pitisha hewa vizuri huwapatia
msongo/stress kuku, na kuku huweza kuanza kudonoana.
9. Uhaba wa vyombo bandani👇
Hii hutokana na kuwa na kuku wengi halafu vyombo vichache vya
chakula , Kwahiyo wakati wa kula lazima watagombania na kudonoana
Kuku wa umri tofauti kuwekwa kwenye banda moja
#Tiba Kinga
#Tiba___ Tumia Protini (Amino Acid) stahiki kulingana na tatizo.
Mfano: (methionine , lysine nk)
#Kinga
_Changanya Proteni kiwango kizuri kwenye chakula cha kuku,chakula cha kuku
kijumuishe virutubisho vyenye asili ya wanyama ambavyo ni chanzo kizuri cha
Proteni
_Hakikisha kuku wako wanakaa kwenye eneo la kutosha . hii inategemea aina
ya kuku na umri wake.
_ Hakikisha kuku wako wana kula chakula na kushiba
_Banda la kuku wako liwe na hewa ya kutosha
_Usiweke kuku umri tofauti katika banda moja
_Uwe unatoa mizoga haraka bandani
_ Wafanye kuku wako wawe wenye furaha , kwa kuwawekea vifaa vya michezo
(bembea).
Pia wafungie mchicha ili wawe bize na kuudonoa huo. Unaweza wafungia mchicha,
kabeji nk
CANNIBALISM KWA KUKU NINI?
Reviewed by BENSON
on
February 02, 2018
Rating:
No comments