UMUHIMU WA MKULIMA NA MFANYABIASHARA WA BIDHAA ZA KILIMO KUTEMBELEA MAONESHO YA WAKULIMA (NANENANE)
Wakulima wengi hujisahau kwa kukusudia au kutokukusudia
kwenda katika maonesho ya wakulima NANENANE ambayo hufanyika kila
mwaka.Kimsingi maonesho haya ni muhimu kwetu wakulima na wafugaji na
wafanyabiashara wa bidhaa za kilimo na mifugo.
BAADHI YA MAMBO MUHIMU AMBAYO
MKULIMA,MFUGAJI AU MFANYABIASHARA WA BIDHAA ZA KILIMO ATAYAPATA KATIKA VIWANJA
VYA MAONESHO.
1. Kupata elimu ya kilimo bora cha mazao mbalimbali ana
kwa ana-Utakutana na wataalam na wakulima wazoefu mbalimbali ambao hutoa elimu
bure kwa wakulima na pia hutoa uzoefu wao katika shughuli za kilimo.
2. Utapata elimu ya ufugaji bora wa mifugo kutoka kwa
wataalam na wafugaji wazoefu.
3. Utapata fursa ya kuziona na kuzitambua mbegu bora mpya
na za zamani za mazao mbalimbali kutoka katika Taasisi za utafiti na
wazalishaji mbegu wakishirikiana na Wakala wa Mbegu za serikali (ASA).
4. Utapata fursa ya kuona mbegu bora za Mifugo ya aina
mbalimbali Mpya na za zamani.
5. Utakutana na wajisiliamali wa mazao ya kilimo na mifugo
na utajifunza mbinu mbalimbali za ujasiliamali kutoka kwao.
6..Utapata fursa ya kukutana na wadau mbalimbali wa kilimo
kama vile
BENKI YA MAENDELEO YA KILIMO YA TANZANIA ( TADB).Ambapo utapata
kutambua na kupata huduma mbalimbali wanazozitoa kwa haraka na wepesi zaidi.
7..Utakutana na watengenezaji wa Pembejeo na Zana
mbalimbali za kilimo na kuona bidhaa zao kama vile zana mbalimbali za kilimo
Kutoka SIDO,VYUO VIKUU,VETA,JKT,Na
wadau wengine.
8.Utakutana na Wadau au Wauzaji Wakubwa Wa Mbegu na madawa
ya Kilimo kama Vile BALTON SEED COMPANY,SYNGENTA
TANZANIA,MONSANTO SEED COMPANY.
9..Utakutana na wasindikaji wa mazao ya kilimo-hivyo
utaweza kujifunza mbinu mbalimbali za uhifadhi,usindikaji,na ufungashaji wa
bidhaa za kilimo.
Kwa kifupi maonesho haya yana umuhimu kwa wakulima wa
za
mani,wapya na wale wanaotaraji kuingia katika kilimo,kiwe kilimo cha mazao ya
chakula au biashara.hivyo ukipata nafasi usisite kutembelea katika maonesho
haya ya nanenane kama vile Morogoro,Arusha,Dodoma,Lindi, Mbeya n.k
UMUHIMU WA MKULIMA NA MFANYABIASHARA WA BIDHAA ZA KILIMO KUTEMBELEA MAONESHO YA WAKULIMA (NANENANE)
Reviewed by BENSON
on
December 30, 2017
Rating:
No comments