SABABU ZA KASUKU/CHIRIKU KUJINYOFOA MANYOYA
Kasuku ni
jamiii ya ndege wapendwao na watu wengi sana hasa maeneo ya mjini. Ndege huyu
hupendwa kwa sababu ana kasumba ya kuwa na rangi zuri za kuvutia, achilia mbali
rangi lakini pia ndege huyu ana sauti ambayo huwa hachisho masikioni mwa watu,
yote tisa ndege huyu ni kivutio cha wengi.
Lakini licha
ya kuwa na sifa hizo, ndege huyu amekuwaa na hulka moja ya kujinyofoa manyoa. Hii
nikutoka na sababu mbalimbalia ambazo nitazieleza hapa na njia za kujikinga ili
kasuku wako asinyofoke manyoa.
Kwa
kuanza tuangalie sababu za kunyofoka kwa manyoa hayo
1. Lishe duni, upweke na kukosa matunzo ya jumla
2. Kama atakuwa anatafuna kucha zako unapomshika
3. Viroboto au utitiri
4. Maambukizi ya bakteria au fangasi
5. Banda dogo sana
6. Lishe yenye vitamini A kwa wingi zaidi
Nini kifanyike ili kuzuia tabia hii ya kunyofoka kwa manyoya
1. Hakikisha ndege wako anapata mlo kamili, unaweza kununua chakula kwenye maduka au ukachanganya mwenyewe baada ya kupata utaalam, apate matunzo yote muhimu na pia asiwe mwenyewe ni vizuri ukafuga dume na jike.
2. Kama unatabia ya kumshika ndege wako hakikisha unavaa kitu cha kukinga asiweze kula kucha zako kama vile gloves
3. Viroboto na uttiiri vidhibitiwe kwa kutumia dawa maalum kama vile akheri powder
4. Maambukizi ya bakteria na fangasi yadhibitiwe mara moja kwa kutumia dawa kama ancobal
5. Ndege wako anaishi kwenye banda lenye ukubwa wa kutosha
6. Punguza vyakula vyenye vitamini A kwa wingi kama vile karoti na mapapai
SABABU ZA KASUKU/CHIRIKU KUJINYOFOA MANYOYA
Reviewed by BENSON
on
December 04, 2017
Rating:
No comments