YAJUE MAGONJWA HAYA AMBAYO HUSHAMBULIA VITUNGUU KWA KIWANGO KIKUBWA.

Related image
Mara nyingi unapojikita katika kilimo cha vitunguu yapo mambo ambayo kiukweli huwa hayakwepi miongoni mwa mambo hayo ni pamoja na magonjwa ambayo hushambulia vitunguu

Magonjwa kama botrytis (kuoza shingo) blue mould na fusarium (kuoza kwa vitunguu) husababisha hasara kubwa kama hayatadhibitiwa kwa kutumia viuatilifu mara unapoona dalili, pia magonjwa kama white rot huchukua zaidi ya miaka 20 kuondoka kama yatavamia shamba lako.

Pia magonjwa kama kutu ya majani husababisha na unyevu mwingi hasa kama mimea itakuwa kwenye udongo unaotuamisha maji au mimea kumwagiliwa jioni au usiku, kumbuka kumwagilia asubuhi tu Ili kudhibiti ugonjwa huu wa kutu mimea ingolewe na ichomwe au utumie viuatilifu vya kuulia fangasi wa mimea

Lakini inashauriwa kufanya mabadiliko ya zao kila baada ya miaka mitano kwa kupanda mazao mengine yasiyo jamii moja kama vitunguu maji, unaweza kupanda maharage, mahindi, karoti na kabichi katika mzunguko huo.


YAJUE MAGONJWA HAYA AMBAYO HUSHAMBULIA VITUNGUU KWA KIWANGO KIKUBWA. YAJUE MAGONJWA HAYA AMBAYO HUSHAMBULIA VITUNGUU KWA KIWANGO KIKUBWA.  Reviewed by BENSON on November 09, 2017 Rating: 5

No comments