UJUE UGONJWA WA KICHAA CHA MBWA
Ugonjwa wa kichaa cha mbwa ni
ugonjwa unaosababishwa na virusi na huwa ni hatari hatua zisipochukuliwa haraka
na dalili kujitokeza na kusababisha kifo.
Ugonjwa huu huwaathiri
wanyama wa kufugwa hata wale wa mwituni, na binadamu hupata ugonjwa endapo atagusana
na mate ya mnyama mwenye ugonjwa kupitia kung’atwa meno au mkwaruzo kutoka kwa
mnyama mwenye ugonjwa.
Dalili za mwanzo za ugonjwa
ni homa, kuhisi kuchomachoma katika eneo lililong’atwa au kukwaruzwa.
Kusafisha eneo lililong’atwa
au kukwaruzwa ndani ya muda mfupi pamoja na kupata chanjo ya kukinga ugonjwa wa
kichaa cha mbwa ni njia thabiti ya kuzuia kupata ugonjwa huu.
UJUE UGONJWA WA KICHAA CHA MBWA
Reviewed by BENSON
on
November 23, 2017
Rating:
No comments