UFUGAJI WA BATA WA ASILI NI FURSA NZURI KIBIASHARA

Related image
Bata ni ndege kama walivyo kuku, kanga na wengine. Bata ana urahisi mkubwa sana kumfuga kwakuwa hana changamoto katika matunzo yake mpaka kupata mazao yake.
Inashauriwa kumfuga bata katika eneo la kubwa kidogo au katika banda maalum kwa wale wasio na eneo kuepuka uchafu unaweza kusambazwa na kinyesi chao.

Chakula cha bata ni Pumba za mahindi lakini pia bata anauwezo wa kula chakula cha aina yoyote ile kama mabaki ya ugali, wali, wadudu nk.
Bata mmoja ana uwezo wa kutaga mpaka mayai 40 kwa zao moja na minimum mayai 15 mpaka 20 kwa zao moja.kwa hiyo bata ana uwezo wa kukuzaliana kwa wingi sana na kukuongezea kipato kwa muda mfupi.

Soko la bata ni kubwa sana ingawa hawaonekani masokoni kwakuwa wafugaji wa bata mijini si wengi kabisa lakini bata mmoja anakadiriwa kufikia shiling elfu 15 mpaka elfu 30. Wateja wengi huwa wanafuata bata zizini baada ya kugundua walipo hivyo hapa inahusika kidogo.

Moja katika uimara mkubwa wa bata huwa hawana magonjwa so ni nadra sana kwa bata 
kufa na kama itatokea kufa basi ama bata amepigwa kichwani au kuungua nk. lakini kwa ujumla ukifuga bata mia unaweza wakuza wote mia bila shaka yoyote hivyo hawana rchangamoto kubwa kibiashara.

Bata hawahitaji madawa na chanjo kama walivyo kuku kwa maana hiyo hutokuwa na gharama za madawa kama ilivyo kwa kuku.


Hebu tuone mchanganuo mdogo wa mradi huu.
Ukinunua bata majike 50 kwa kuanzia na madume 10.
50 × 15,000= 750,000/= Majike
10 × 20,000= 200,000/= madume.
Jumla itakugharimu kama sh. Milioni moja. Pamoja na usafiri.
Hapo chakula chao kwa bata 50 wanauwezo wa kula pumba debe 10 kwa mwezi na kila debe ni wastani wa sh. 3000 Elfu tatu. Chakula kwa mwezi kitakugharimu sh. 30,000/= Elfu thelathini hivi.
Bata majike 50 kila mmoja akitaga mayai ya chini 20 ndani ya mwezi wa kwanza utakuwa na uhakika wa kupata bata
50 × 20 = 1,000. Bata elfu moja. Ambao utakuwa na uhakika kwamba lazima wakue wote kwa sababu ni wako free from magonjwa.
hivyo ukiwa na bata elfu moja ndani ya miezi 6 watakuwa tayari kuuzwa na kutaga upya. 
UFUGAJI WA BATA WA ASILI NI FURSA NZURI KIBIASHARA UFUGAJI WA BATA WA ASILI NI FURSA NZURI KIBIASHARA Reviewed by BENSON on November 25, 2017 Rating: 5

No comments