ZIJUE TABIA WALIZONAZO KUKU AINA YA CHOTARA.
Habari za wakati huu wapendwa wasomaji wetu ,leo
ningependa kuwaalika kujifunza kitu kidogo kuhusu utafauti wa kuku chotara na
kuku wa asilia.
ZIFUTAZO NI TABIA WALIZONAZO KUKU CHOTARA.
1.
Kuku chotara hutaga mayai mengi zaidi
ukilinganisha na kuku wa asili. Kuku chotara hutaga mayai 220-280 kwa mwaka
kulingana na ubora wa chakula na mfumo mzima wa ufugaji.
2.
Tetea wa chotara hula kiasi cha 6.8kg
kwa muda wa miezi mitano na kuweza kufikia uzito wa 1.8kg kwa kipindi hicho.
3.
Jogoo chotara huweza hula kiasi cha
6.8kg kwa muda wa miezi mitano na kuweza kufikia uzito wa 2.6 kwa muda huo.
4.
Matetea chotara huanza kutaga ndani
ya muda wa miezi mitano mpaka sita kutegemea na utunzaji na vyakula wanavyopewe.
5.
Ili kuku hawa watage sana wanatakiwa
kula angalau 122g kwa siku za chakula kizuri ili kuweza kutaga kwa muda mrefu.
6.
Kuku hawa wataanza tabia ya kudonoana
kama wasipopewa chakula kizuri na chenye virutubisho vya kutosha pamoja na
madini.Kuku hawa hudonoana sana na wakati mwingine hupelekea vifo na vidonda
ZIJUE TABIA WALIZONAZO KUKU AINA YA CHOTARA.
Reviewed by BENSON
on
September 02, 2017
Rating:
No comments