ZIJUE MBEGU BORA ZA MAHINDI
Habari
za muda huu mpenzi msomaji wetu, bila shaka u mzima wa afya tele, nichukue furs
hii adhimu kukuarika wewe katika somo letu la leo, somo letu la leo linatokana
na maswali ambayo huwa tunaulizwa na wasomaji wetu, wengi huuliza ipi ni mbegu
bora ya mahindi ili nipate mavuno mengi.
Ukweli
ni kwamba mbegu bora ya mahindi ina
mchango mkubwa sana katika kupata mazao mengi na yenye thamani kubwa. Bila kua
na mbegu bora sidhani kama unaweza kupata mazao bora kabisa. Hivyo kila wakati
ni vyema akajifunza mbinu bora za kupata mbegu bora ili uweze kupata mazao
mengi na bora pia.
kitaalamu kuna mbegu aina mbili japo zina majina mengi mengi kutokana na
makampuni na qulity kidigo zimetofautiana mfano kuna pana,seedco, star na
zingine nyingi.
Lakini kila kanda kuna aina ya mbegu ambazo zinakubali sana katika ukanda
husika bado sijapata takwimu sahihi ya kila mkoa na aina ya mbegu ambayo inakubali
sana.
ila ningependa ndugu msomaji uelewe kitu kimoja ambacho ni cha msingi sana.
Kuna
aina mbiili za mbegu ambazo ni:
AINA ZA MBEGU YA MAHINDI
i/ Mbegu ndefu
ii/ Mbegu fupi
MBEGU NDEFU
Hizi ni mbegu ambazo zinakaa mda mrefu kidigo kuliko mbegu fupi, mbegu hizi
hukaa siku 100 hadi siku 120 hapo ndipo zinakua tayari kuvunwa. Lakini ni mbegu
ambazo zinakua ndefu sana kwa kimo, zinamabua makubwa sana pamoja na
punje ambazo ni kubwa pia. mfano hybrid,pana
ndefu
MBEGU
FUPI
Hizi ni mbegu hazichukui siku nyingi sana mpaka kukomaa zinachukua siku
75 hadi siku 90. Lakin zinakua na punje ndogo kutokana na aina na zinakua na
bua fupi pia.
lakini hizi ni mbegu ambazo ni nzuri kwa wakulima ambao wanalima kwa ajili ya
biashara, kwani ni za muda mfupi na pia biashara yake inalipa zaidi.
mfano star na stuka.
ZIJUE MBEGU BORA ZA MAHINDI
Reviewed by BENSON
on
September 11, 2017
Rating:
No comments