HAYA NDIYO MAGONJWA AMBAYO HUWASUMBUA SANA KUKU

Image result for kuvimba macho kwa kuku

Ufugaji wa kuku kuna changamoto kubwa ya kuku kupata magonjwa ambayo yataathiri ukuaji wake au kuku kufa. Magonjwa mengi kuku huyapata kutokana na banda kutokuwa safi, kuingia kwa ugonjwa katika banda, kutofuata taratibua za kinga na magonjwa ya mlipuko.

Haya ni kati magonjwa ambayo kuku huyapata katika vipindi tofauti vya ukuaji wake


  • Kuharisha damu

Dalili ya kuku kuharisha damu kama vile kuku kupata kinyesi cha damu, kuku kushuka mabawa na kuku kutochangamka.

Kutibu; usafi wa banda la kuku, kuwatenga kuku wenye homa na vile vile tumia dawa ya amporium, Typhoprim, Esb3 n.k


  • Kideri (Newcastle)

Husababishwa na virusi na dalili zake kama kuku kupumua kwa shida, kuku kuhara na kuku hufa wengi kwa mkupuo.

Kutibu; kuku wachanjwe katika juma la kwanza, baada ya wiki mbili, baada ya kufikisha miezi mine na kila baada ya miezi miwili au mitatu.


HAYA NDIYO MAGONJWA AMBAYO HUWASUMBUA SANA KUKU HAYA NDIYO MAGONJWA AMBAYO HUWASUMBUA SANA KUKU Reviewed by BENSON on May 16, 2018 Rating: 5

No comments