KILIMO BORA CHA MIWA
Kilimo cha miwa ni kilimo chenye tija kwa mkulima, kilimo hiki
kinaweza kufanywa na mtu yeyote yule aidha awe ameajieiwa au laaa! Jambo la
msingi ni kuhakikisha anajitoa kikamilifu katika kuhakikisha unawekeza akili yake katika kulima kilimo
hiki.
Kuna aina kuu 2 za miwa katika mbegu za miwa zilizo shamili sana
ambazo ni:
1. Bungala
2. Miwa myekundu.
Unachotakiwa kufanya katika kulima kilimo hiki ni, Kwanza kabisa
tafuta ekari moja ya shamba kisha anza maandalizi lakini zingatia kupuguza
matumizi makubwa ya pesa kadri iwezakanavyo yaani kwa shughuli nyinginezo
ambazo unaweza kuzifanya mwenyewe ni vyema ukazifanya ili kupunguza matumizi
makubwa ya pesa mfano kulima, kupiga dawa, kupalia n.k
Tafuta mbegu ya miwa ya Bungala miwa hii ni laini sana na ni
rahisi kuichana kwa kutumia meno, baada ya kupata miwa hii kata vipande vipande
vya pingili tatu tatu .Kumbuka kwamba miwa ni rahisi sana kushambuliwa na mchwa
pale tu inapokuwa imepandwa.
Ili kuzuia isiliwe na mchwa nenda katika maduka ya kilimo na
ununue moja wapo ya madawa yafuatayo:-
1. TAP 4% GR Tumia gram 100 za dawa kwa lita takribani 20 za
maji kisha nyunyizia katika mashina ya miwa.
2. Taniprid 25 WG. Tumia gram 100 za dawa kwa lita takribani 20
za maji au pia unaweza kuweka kijiko kimoja cha chai katika kila shina.
3. Imida Gold Mls 20 kwa lita 20 za maji na unyunyizie shinani.
4. Gammalin 20. Tumia
gram 100 kwa lita takribani 20 za maji. Na unyunyizie katika vipande vya miwa
au chovya vipande vya miwa katika maji hayo yaliyo na Gammalin 20 na ndipo
uende ukavipande shambani kwako.
5. Gladiator FT.
6. Stom
Mambo yakufanya:
Zingatia kama utatumia aidha Gladiator au Gammalin au Stom,
chukua ndoo ya maji ya lita 20 kisha uichanganye na dawa uliyoinunua kisha
chukua kipande cha muwa na kukizamisha ndani ya maji hayo na baadae uende
kuipanda shambani kwako, hivyo uewezekano wa miwa yako yote kuote utakuwa ni
mkubwa sana maana shida kubwa ni mchwa na hapo tayari utakuwa umeidhibiti.
UPANDAJI WA
MIWA
Hakikisha unapokuwa unapande miwa yako acha nafasi ya mita moja
(1m) kati ya mche na mche pia hakikisha una acha nafasi ya mita moja (1m) kati
ya mstari na mstari. Kumbuka awali tulisema katakata muwa wako kupata vipande
vilivyo na vipingili vitatu vitatu, hivyo sasa unapokuwa unapande miwa hii
hakikisha hizo pingili zote 3 zimezama ndani ya ardhi na kipande kidogo tu ndio
kibakie juu ya uso wa ardhi na mche wako huo unapoutumbukiza kwenye ardhi uwe
umelala wastani wa nyuzi 30.
Zile pingili katika muwa wako kumbuka ndipo sehemu hasa miwa
inamokuwa inachipuka na kuota. Mantiki ya kuacha nafasi kubwa kati ya mche na
mche ni kwa sababu hilo shina lako moja ulilolipanda linaweza likachipua
vijimiwa vingine zaidi hata ya ishirini kama ukiliacha shina liendelee kuzaa tu
kwa kadri linavyotaka na hatimaye shamba lako litakuwa msitu hata usiopitika.
Lakini kibaya zaidi ni kwamba miwa yako itakosa afya njema na
mwisho wa siku miwa yako haitakuwa bora hata bei haitakuwa nzuri pindi
utakapoamua au wakati wa kuuza utakapofika. Hivyo unashauriwa kuacha miwa kati
ya tano mpaka kumi lakini mfano ukiacha miwa mitano katika shina moja ni dhairi
hewa na mwanga vitakuwa vya kutosha shambani lakini hata chakula na virutubisho
vingine kwa miwa hiyo vitakuwa lukuki na sio vya kung’ang’aniana hivyo mwisho
wa siku utapata miwa mirefu na minene ambayo sokoni itakuwa na mvuto mkubwa kwa
wateja.
Mfano chukulia kwamba umelima ploti ndogo tu ya upana mita 50
kwa urefu mita 70, kumbukumbu namna ya upandaji miwa kama tulivyozungumza hapo
awali umbali wa mita moja moja kwa kila shina. Hivyo kwa ploti ya shamba hili
utakuwa na miche au mashina uliyopanda kiasi cha 70×50=3500 (mashina elfu tatu
na mia tano) sasa chukulia kwa hesabu rahisi kwamba kila shina umeruhusu miwa
mitano tu ndio ikuwe pale maana yake kwa mashina 3500 utazidisha mara 5 ambapo
itakuwa 3500×5= 17,500 hiyo ndio itakuwa jumla ya miwa itakayovunwa shambani.
Kwa tafiti zilizofanywa zinaonesha kama hautaki shida na
unahitaji pesa ya haraka haraka sana huko huko shamba, basi unaweza ukajumlisha
miwa yako kwa bei ya chini sana yaani tukadilie vile kwamba tunahitaji pesa ya
haraka so tuuze muwa mmoja kwa bei ya jumla ya 300 hivyo jumla ya pesa
utakayoipata itakuwa 17,500 × 300 = 5,250,000 (milioni tano laki mbili na
nusu). Hiyo ni pesa ya haraka haraka huko huko shambani .
Ila kama ukiweza kusogea zaidi na kuuza kwa faida maana kama
umeweza kupigana mpaka kuweza kuikuza ni dhairi kwamba unastahili kupata faida
iliyo njema kwako hivyo ni muhimu kuangalia masoko yamekaaje pande zote za
miji, ila kama utaweza kuifikisha Dar es Salaam ambako kiuhalisia soko lake ni
kubwa sana .
Kama ukienda Kariakoo bei ya rejareja kwa muwa aina ya bungala
wenye wastani wa urefu mita moja na robo bei yake ni 5,000 lakini ukienda
mtaani kwa muwa huo huo aina ya bungala mfupi kidogo bei yake inakwenda mpaka
3,500 hivyo chukulia kwamba umeweza kufikisha Dar es Salaam huo mzigo wako wa
miwa, hivyo mapato yako kama utaamua uuze kwa bei ya jumla ya 1,500 kwa kila
muwa hivyo kiasi cha fedha utakachokipata kitakuwa ni sawa na idadi ya miwa
yako zidisha bei ya kujumlishia yaani ingekuwa 17,500 × 1,500= 26,250,000 hii
ni pesa utayoipata kwa halali kabisa wala haujamzulumu mtu.
Hapo umelima ploti ndogo tu, sasa chukua pengine umelima ekari
moja na kwa shamba la miwa ekari moja kiwango cha chini kabisa cha wewe kuvuma
miwa yako ni jumla ya miwa 24,500. Sasa chukulia kama umeweza kuipeleka Dar es
Salaam maana yake utapata jumla ya 24,500 × 1,500= 36,750,000. Sasa mfano ndo
ukalima ekari 4 hadi 5 hapo ni hakika unatoka katika kundi la uchumi wa chini
na kuingia katika uchumi wa kati. Jamani bado hatujachelewa kungali bado fursa
ziko kinachohitajika hapa ni kuthubutu tu, Mungu akubariki unapoyatafari haya
lakini pia pindi ukifanikiwa usimsahau Mungu maana yeye ndiye nguzo ya
mafanikio yako yote.
KILIMO BORA CHA MIWA
Reviewed by BENSON
on
August 08, 2017
Rating:
HIyo imekaa vizuri,mbegu za miwa hiyo ya Bungala zinapatikana wapi?
ReplyDeleteHujaonyesha inachukua muda gani kupanda hadi kuvuna na wakati gani unaofaa kwa kuandaa shamba hadi kuapanda,na ni kwa umwagiliaji au kwa kutegemea mvua.
ReplyDeletemuda ni miezi6 na inategemea sana mvua
ReplyDeleteInasati sana kwenye mikoa gan??(vipi kuhusu Pwani),Ukihitaji mbegu ya bungala inapatikana wap??
Deleteina maana ukimwagilia mapema ina wahi zaid
ReplyDeletehakuna mbolea za viwandani zinazotumika kwa miwa na je kiasi gani cha samadi kinafaa kulifanya shina moja la miwa litoe miwa ya kutosha
ReplyDeleteHakika nimevutiwa na kilimo hiki cha miwa napenda kuuliza miwa nilazima ilimwe bondeni au hata karbu na bonde inafaa
ReplyDeleteMashamba ya miwa yanapatikana wapi, nijuze 754711153, naitaji nami nianze hii kitu, na ikiwezekana hata karibu na kiwanda cha sukari ili nipate soko la karibu.
ReplyDelete