NAMNA YA KUTUNZA KUMBUKUMBU KATIKA UFUGAJI WA KUKU.
Kwa
mfugaji yeyeote yule wa kuku ni lazima aweze kujijengea utaratibu wa kuandika
na kutunza kumbukumbu wa kuku wake. Usipo kuwa na utaraitibu huo, jiandae
kusikia ule usemi usemao."mali bila daftari hupotea bila habari".
Hivyo ni vyema ukiwa na mradi wowote wa
ufugaji ni vema ukiwa unaweka kumbukumbu za kila siku au kwa kila wiki.
Katika kutunza kumbukumbu za ufugaji
kuna mambo muhimu ya kuyazingatia kama ifuatavyo:-
1.
Kumbukumbu za kuku na uzalishaji
Hii
ni kuanzia unapowapokea hadi kuwatoa bandani. Hapa unapaswa kila siku
uwaangalie kuku wako ili kujua wanahali gani na ni wangapi waliopo, hapo
utaelewa kama kuna ugonjwa wa kutibu au tahadhari gani zichukuliwe.
kama ni kuku wa mayai basi kujua idadi ya mayai wanyotaga kila siku, ili uweze
kujua asilimia za utagaji na uweze kupima kiwango chao cha utagaji.
2. Kumbukumbu za cahanjo.
Weka kumbukumbu za chanjo dhidi ya magonjwa mbalimbali kama vile mdondo
(Newcastle), gumboro, ndui na magonjwa mengine.
3. Kumbukumbu za afya.
Hapa unarekodi kila aina ya ugonjwa uliotekea bandani, idadi ya walioathirika,
waliotibiwa, waliopona na waliokufa. Gharama za matibabu nazo pia ziwekwe
kwenye kumbukumbu.
4. Gharama za vifaa na chakula.
Vifaa vyote unavyonunua kwa ajili ya ufugaji ni lazima viorodheshwe na viwekwe
kwenye kumbukumbu, na gharama za chakula kuanzia unapoingiza kuku hadi
unapowatoa iwekwe kwenye kumbukumbu pia.
MUHIMU: Njia rahisi ya kutunza kumbukumbu ni kununua daftari na kutengeneza
majedwali yanayoonesha vipengele tajwa hapo juu.
NAMNA YA KUTUNZA KUMBUKUMBU KATIKA UFUGAJI WA KUKU.
Reviewed by BENSON
on
August 07, 2017
Rating:
No comments