USINDIKAJI WA MBOGA ZA MAJANI KWA NJIA ASILI

Image result for mboga za majani
Ukashauji wa mboga za majani ni njia ambayo inatumika sana maeneo ya vijijini lakini si vibaya ikianza pia kutumika maeneo ya mijini kwani ni njia nzuri sana. Kwa maneno mengine njia hii ni usindikaji wa mboga za majani. Na moja kati faida kubwa ambayo utaipata mara baada ya kukausha mboga hizi ni kwamba mboga hizi zinaweza kukaa kwa muda mrefu hivyo kusaidia wakati wa mboga zinapokuwa hadimu.


Mambo ya msingi ya kuzingatia wakati wa kukusha mboga za majani ni ifuatavyo:

1.    Chuma mboga nyingi katika bustani yako. Hajalishi ni mboga za aina gani.

2.    Hatua inayofuata ikatekate vipande vidogo vidogo.


3.  Baada ya hapo chemsha katika maji ya moto. Lakini jambo la kuzingatia ni kwamba chemsha mpaka ibadili rangi yake, isiwe katika hali ya ukijani.

4.    Mara baada ya kuchemka na kujiridhisha kwamba imeiva vizuri. Epuka kisha subiri kwa muda fulani mpaka ipoe vizuri.


5.    Ikisha poa vizuri  chukua kitu ambacho kitakusaidia kuianika mboga hiyo mpaka ikauke vizuri.

6.    Mara baada ya kukauka vizuri ni kwamba unaweza ukaiifadhi sehemu safi ili ije kuliwa hapo baadae.
USINDIKAJI WA MBOGA ZA MAJANI KWA NJIA ASILI USINDIKAJI WA MBOGA ZA MAJANI KWA NJIA ASILI Reviewed by BENSON on June 19, 2018 Rating: 5

No comments