UFAHAMU UMWAGILIAJI WA MATONE (DRIP IRRIGATION SYSTEM)
Mfumo wa umwagiliaji
wa matone (Drip irrigation system) unafanya kazi kama zile drip za hospital za
kuongezewa maji au damu ambazo huwa tunaziita drip... wanasemaga mtu
katundikiwa drip ya maji.
Vitu vinavyotengeneza mfumo huu.
1. Pump...
Hii inafanya kaza ya kuvuta maji kutoka kwenye chanzo cha maji na kupeleka
shambani direct au kwenye tank au water resevour kwa kuhifadhi.
2. Filters/
chujio... Filter zinachuja maji ili takataka na particles nyingne siziingie
kwenye mfumo wa umwagiliaji na kuleta shida kama za kuziba pipes na emmiters Emmitters
ni visehemu vya kutolea maji kwa ajili ya kumwagilia.
3. Back
wash controller/ back flow contorller ni vivalve vinavyozia maji kurudi nyuma
ya mfumo hasa mgandamizo wa maji ( pressure) inapokuwa ndogo. Maji yanatakiwa
yawe na uelekeo mmoja tu (Unidirection). Hizi ni kama valves za mishipa ya vein
zinavyozuia damu isirud nyuma.
4. Pressure
regulator au control valve... inafanya kaz ya kucontrol pressure ya maji
inayoingia kwenye pipes... ni muhimu sana kuregulate pressure maana ikizidi tu
unaweza kukuta sio drip tena ila pipes au tape zimeburst zote ukazimia.
5. Water
tank/resouvr au chanzo cha maji... kazi ni kusupply maji kwenye drip... lazima
maji yawepo ndio uwe mfumo wa umwagiliaji.
6. Main
line/ pipe ni bomba kubwa linalotoa maji kwenye tank au kwenye source nyingine
kwenda shambani kwa ajili ya kusambazwa. 7.Small poly tubes/tapes hizo ndio
zileee zinasambaza maji shambani sasa na ndio zenye vitobo vya kudodondoshea
maji sasa.
Kuna connectors pia ambazo
zinaunganisha hizo tubes na pipes. Pia kuna gate valves... hizi zinasaidia
kumwagilia shamba kwa awamu... yani unaweza kumwagilia nusu shamba kwanza
ukaendelea na nusu baadae. Gate valves Ikifungwa zinazuia maji kwenda eneo moja
na kuruhusu eneo jingine hasa kama maji yana pressure ndogo.
Kuna source ya power
kama umeme au solar kwa ajili ya pump lakin pia unaweza kutumia mafuta tu
Naombeni niendelee na faida za kutumia mfumo huu wa
umwagiliaji.
1. Matumizi mazuri ya
maji
Mara nyingi wakulima
hawajui kama kumwaga maji hovyo ni tatizo as long as yapo
Sasa drip inapunguza
kupotea maji unnecessarily kwa sababu inadondosha maji kwenye mmea tu.
Kwa wenzangu wa kanda
ya kati ambao kuna shida ya maji wataelewa kirahisi au kama unatumia ya DAWASCO
yanye mita mtaelewa zaidi
2. Kwa
sababu mfumo huu unamwagia maji kwenye shina la mche tu... unasaidia sana kupunguza
shida ya magugu shambani... wakat mmea unapata maji tena ya kutosha magugu
yanalala njaa inapunguza usumbufu na gharama za palizi.
Ukimwagia kienyeji kwa
sababu unamwaga maji mengi kwa wakat mmoja... yanapotea haraka sana na mengine
ndio yanaenda kustawisha magugu
3. Matumizi mazuri ya
mbolea... hapa patamu
Kwa mbolea za dukani
zinazoyeyuka kwenye maji... water soluble...unaziweka kwenye tank zinayeyuka
(kutengeneza solution) na then zinaenda kwenye mimea kwa kupitia matone
yanatoka kwenye tubes... once again magugu yanalala njaa .
Tofauti na kumwaga
shimon then unamwaga lita 5 za maji mbolea inayeyuka na kupoletlea pembeni
magugu nayo yanasherehekea
4. Haki sawa kwa kila
mmea.
Mfumo wa umwagiliaji
wa matone unatoa kiwango sawa sawa cha maji na mbolea kwa mimea yoooote
shambani. Yami mmea ambao upo karibu na chanzo cha maji unapata kiasi cha maji
sawa sawa na mmea ambao upo hukooo mwisho wa shambani... kwa sababu hii basi
mazao yanatoka mengi uniform kama matikiti mengi yanakua makubwa na
yanayokaribiana sana size.
Tofauti na umwagiliaji
wa kawaida ambapo mmea karibu na kisima ndio umapendelewaaa halafu ile ya
kwenye margin inakonda kwa sababu watu wanachoka sana pia kubeba ndoo nenda
rudi.
5. Inapunguza gharama ya nguvukazi na kupunguza chamhamoto ya
nguvu kazi
Watu wengi wanaishi
mjini wana mashamba bush na vijana wanawadanganya sana kuwa wamemwagilia kumbe
sio au wamemwagilia kwa kumbe wamerashia tu... hii system kwa sababu ni ya
kufungua tu na kufunga bomba hata mtoto wa darasa la kwanza anaweza kuelekezwa
kufungua na kufunga bomba kama ina kijana wa kazi safi angalau kwa sababu
hatumii nguvu kubwa sio rahisi kukudanganya.
5. Mfumo
wa drip unapunguza trembling/ kukanyaga kanyaga shamba ambapo kunasababisha
compaction ya shamba na kupunguza circulation ya hewa ardhini.
6.
KUONGEZA
UZAAJI.
Nimeandika kwa herufi
kubwa kabisaaaaaa....
Drio irrigation bwana
inaongeza uzaaji almost 3-4 times normal irrigation... natumia kwenye matikiti
maji... kwa kawaida nilipata tani 4 kwa heka na tani 12 kwa drip. Hii
inasababishwa na usawa kwenye maji na mbolea.
7.
Drip zinapunguza mmomonyoko wa ardhi... tofauti na kumwagilia
kienyeji au kwa mitaro
Yan kama unatumia drip
na ukaweka matandazo ya plastic (Plastic mulch) umemaliza... no palizi... no
energy... high yield... grt production
Pia mfumo wa drip ni
portable ambao unaweza kuutumia hata kwenye shamba la kukodi na kuutoa unaweka
kwenye kirikuu mpaka home... kuwe na chanzo kizur cha maji tu
Diadvantages
- Mfumo huu ni ghali
kidogo hawa kwa wanaoanza kwa sababu roll moje ya mita 2000 inauzwa 1.8M mpka
3.6 ambayo inatosha heka moja tu ya matikiti maji... japo otakisaidia sana
kuweka mbegu nyingi shambani na kuvuna sana sana sana
Disadvantage nyingne
ni kwamba installation yake inahitaji utaalami kidogo kitu ambacho kinaongeza
gharama kwa sababu sio kila mtu anaweza kufunga drip
UFAHAMU UMWAGILIAJI WA MATONE (DRIP IRRIGATION SYSTEM)
Reviewed by BENSON
on
February 27, 2018
Rating:
No comments