NAMNA YA KUWALISHA KUKU WA MAYAI
Kuku wa mayai ili watage vizuri wanatakiwa walishwe chakula
bora kwa utaratibu unaotakiwa, ukiwazidishia au kuwaongezea hawatotaga vizuri.
Wanatakiwa walishwe kati na kati kulingana na umri kama ifuatavyo:-
UMRI WA WIKI
1 -2
Katika umri huu wanapewa chakula aina ya "Super Starter" kwa
ajili ya kuwatengenezea kinga mbadala ili waweze kuhimili mikiki mikiki ya
vijidudu vya magonjwa kadri wanavyoendelea kukua, wanapewa chakula hicho kwa
kiwango maalum kama ifuatavyo:-
Wiki ya 1: Gramu 12 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 2: Gramu 22 kwa kuku mmoja kwa siku moja
UMRI WA
WIKI 3 - 8
Hapa wanakuwa bado ni vifaranga na wanapewa
chakula aina ya "Chick Starter" kwa ajili ya kuendelea
kuwajenga miili yao waweze kupoekea virutubisho vizuri, hii inatokana na kwamba
kuna baadhi ya viinilishe vinafanya kazi ya kumeng'enya chakula na kupatikana
viinilishe vingine, kwahiyo vikikosekana katika mwili wa kuku basi hata wale
chakula gani bora, hawawezi kutoa mazao bora, lakini kwa kuwapa "Chick
Starter" itawapelekea kuwa na virutubisho hivyo muhimu. Kiwango na
ulishaji wake ni kama ifuatavyo:-
Wiki ya 3: Gram 27 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 4: Gram 32 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 5: Gram 38 kwa kuku mmoja kwa siku
moja
Wiki ya 6: Gram 42 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 7: Gram 46 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 8: Gram 50 kwa kuku mmoja kwa siku moja
UMRI WA
WIKI 9 - 18
Katika umri huu kuku wanapewa chakula aina
ya "Grower Mash" kwa ajili ya kuwakuza na kuwajenga mfumo wa
uzazi kwa maandalizi ya utagaji. Kiwango cha chakula kinategemea na wiki kama
ifuatavyo:-
Wiki ya 9: Gram 56 kwa kuku mmoja
kwa siku moja
Wiki ya 10: Gram 62 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 11: Gram 64 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 12: Gram 66 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 13: Gram 68 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 14: Gram 74 kwa kuku mmoja kwa siku
moja
Wiki ya 15: Gram 74 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 16: Gram 80 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 17: Gram 82 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 18: Gram 88 kwa kuku mmoja kwa siku moja
UMRI WA
WIKI 19 - 40
Huu ni umri ambao kuku wanataga kwa kiwango
kikubwa sana (85% hadi 100%) hali ambayo inawafanya kutumia nguvu nyingi mno,
hivyo hupewa chakula aina ya "Layers Phase 1" kwa ajili ya
kufidia nguvu ya ziada wanayotumia ili waendelee kutaga kwa kiwango hichohicho.
Ulishaji wake ni kama ifuatavyo:-
Wiki ya 19: Gram 92 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 20: Gram 102 kwa kuku mmoja kwa siku
moja
Wiki ya 21: Gram 108 kwa kuku mmoja kwa siku
moja
Wiki ya 22: Gram 114 kwa kuku mmoja kwa siku
moja
Wiki ya 23: Gram 116 kwa kuku mmoja kwa siku
moja
Wiki ya 24: Gram 120 kwa kuku mmoja kwa siku
moja
Wiki ya 25 - 40: Gram 130 kwa kuku mmoja
kwa siku moja
UMRI WA
WIKI 41 - 80
Katika umri huu kuku wanakuwa wameanza kuchoka na huanza kutaga kwa kiwango cha
kawaida (65% hadi 75%) hivyo hupewa chakula aina ya "Layers Phase 2"
kwa ajili kuendeleza (maintain) kiwango chao hicho kwa muda mrefu. Kiwango chao
ni "Gram 130 kwa kuku mmoja kwa siku moja".
NB: Kuanzia wiki 81 na kuendelea unaweza kuwauza
na kuweka kuku wengine.
NAMNA YA KUWALISHA KUKU WA MAYAI
Reviewed by BENSON
on
January 16, 2018
Rating:
No comments