KANUNI ZA KILIMO BORA CHA PAPAI


Papai ni moja ya tunda mashuhuli linatumika kwa kiasi kikubwa nchini Tanzania. Pia tunda hili linaweza kuwa na faida mbali na afya, katika kukuza uchumi wa mkulima wa zao hili. Pia linawezakuwa chanzo kikubwa cha pesa za kigeni kwa kuuza nje ya nchi.

Uzalishaji wa papai nchini Tanzania ni kwa kiasi kidogo ukilinganisha na mahitaji ya watumiaji, hivyo inahitajika nguvu zaidi katika uzalishaji wa zao hili.

Kijinsia mpapai umegawanyika katika aina tatu.

  • Mpapai wenye maua kiume tu. 
  • Mpapai wenye maua kike tu. 
  • Mpapai wenye maua ya jinsia zote (Hermaphrodite papaya). 


Katika uzalishaji kila aina ya mpapai unahitajika. Mpapai wenye maua ya kiume uhitajika katika urutubishaji wa mpapai wenye maua ya kike ili kupata matunda. Mpapai wenye maua ya jinsia zote hauhitaji mpapai wenye maua ya kiume maana uweza kujirutubisha wenyewe.

Kutokana na jinsia ya maua mpapai huweza kutengeneza matunda yenye maumbo tofauti. Matunda yanayotengenezwa kutoka katika mpapai wenye maua ya kike tu huwa na umbo la mviringo zaidi au yenye umbo la yai na matunda yanayotokana na mpapai wenye maua ya jinsia zote mbili huwa na umbo la refu zaidi au umbo la pear.

UZALISHAJI WA ZAO LA PAPAI.
Miche ya mpapai Katika uzalishaji wa miche ya mpapai kuna aina mbili za mbegu ambazo huweza kutumika:

1. Mbegu za Kawaida (Local seeds).
Hizi ni mbegu ambazo huweza kukusanywa toka katika mipapai ya kienyeji. Aina hii ya mbegu ni vigumu kujua kati ya mbegu ni ipi dume, jike ama yenye jinsia zote.

Hivyo itakulazimu kung'oa baadhi ya mipapai dume pindi itakapo weka maua hivyo kuacha majike na yenye jinsia zote mbili. Mapapi yenye maua ya kiume uachwa kwa uwiano wa 1:50 ya mipapai yenye maua ya kike.

2. Mbegu chotara (Hybrid seeds)
Aina hii ya mbegu ni nzuri kwa sababu mbegu zote huwa ni ya mipapai nyenye maua ya kike na ya kiume pamaja (Hermaphrodite papaya)na pia hukua haraka na kutengeza miti mifupi yenye uzao mkubwa ukilinganisha na ile ya kienyeji. Mfano. Red royolen F1 au MALAIKA F1.
UPANDAJI.

Panda mbegu moja tu kwa kila kiriba chenye udongo uliochanganywa vizuri na kujazwa robo tatu. Kisha weka viriba vyako venye mbegu chini ya kivuri kisha mwagilia maji. Baada ya kumwagilia unaweza pulizia kiasi kidogo cha kiuwatilifu (fungicide & Insecticide) kwenye udongo wako ili kuzuia wadudu na fungasi wasiathili mmea wako.

Mbegu ya papai uweza chukua siku 8 hadi 15 kuchomoza toka kwenye udongo. Hivyo hakikisha unamwagilia maji kila siku kwa kiasi. Usimwagilie maji mengi sana. Mpapai huweza kuamishwa toka kwenye kitalu baada ya wiki sita hadi nane.

KITALU CHA MIPAPAI NA BAADHI YA SABABU MUHIMU ZINAWEZA ATHILI UKUAJI WA MIPAPAI.
Mpapai upendelea zaidi udongo unaopitisha maji na mzuko wa hewa kirahisi na wenye makadilio ya Ph 6.5. Inapowezekana zuia kupanda mimea yako kwenye udongo wa mfinyanzi na wenye magadi. Kiasi cha maji kilichopo kwenye udongo huweza kuonyesha ukubwa wa matunda.

Eneo lenye udongo wenye unyevunyevu mwingi huweza tengeneza matunda makubwa na yaliyoja maji maji na eneo lenye unyevunyeku kidogo hutengeneza matunda madogo na magumu. Mpapai hawezi kuvumilia upepo mkali, maji yaliotwama pamoja na ukame.

UANDAAJI WA SHAMBA.
Njia ya kuandaa shamba itategemea na eneo (topography), aina ya udongo, vifaa vinavyotumika kuhudumia shamba. Nafasi kati ya mmea na mmea ni mita 2 hadi 2.5 na kati ya mstari na mstari ni mita 2.5 hadi mita 3.

Andaa mashimo yenye upana na urefu wa sentimita 60. Tenga udongo wa chini na wa juu. Kisha changanya udongo wa juu na mbolea ya samadi. Katika kurushisha kwenye shimo tanguliza udongo ulochanganywa na mbolea ya samadi chini na juu malizia na udongo uloutoa chini wakati wa kuchimba shimo.

Kiasi cha mmea huwa kati ya 1000 hadi 2000 kwa hekta (400 hadi 800 kwa ekari) Kupanda mimea shambani Baada ya hizo wiki sita hadi nane hamishia mimea yako shambani. Kazi ya uhamishaji wa mimea ufanyika wakati wa asubuhi sana, jioni ama kukiwa na mawingu ili kuzuia madhara ya jua kwa mimea.

UWEKAJI WA MBOLEA. 
Zuia matumizi ya mbolea zenye chlorine maana mipapai uathiliwa na chlorine. Wiki moja baada ya kuhamisha miche yako weka mbolea gramu 28 kwa kila mche. Tumia mbolea yenye phosphate kwa kaisi kikubwa.

Mfano; - 12:24:12. (NPK) Baada ya hapo kila baada ya wiki mbili weka mbolea yenye Nitroni kwa kiasi kikubwa kiasi cha gramu 56 kwa mmea. Mfano. 20:10:10 (NPK) Potassium inahitajika kwa maua na kuweka matunda hivyo tumia mbolea yenye potassium kiasi kikubwa mara baada ya kuona mmea wako umeanza kuweka maua, kiasi cha gramu 114 cha mbolea huitajika, fanya hivyo kila baada ya mwezi. Mfano. 12:12:17 + 2 (NPK) . Weka mbolea ya majani yenye virutubisho vidogo vidogo ikiwemo boron kila mweze. Boron ni mbolea ya muhimu katika kupata matunda mazuri.

UMWAGILIAJI.
Maji ni sehemu ya muhimu sana katika maisha ya mmea kwa kipindi chote. Maji ni ya muhimu sana katika kuweka maua, matunda na ukuaji wa matunda. Katika ukuaji wa matunda hakikisha unaweka lita 23 kwa kila mmea kwa wiki.

Magugu Hakikisha unazuia magugu kipindi cha mwanzo ili kuzuia ushindani kati ya mimea na magugu kwa virutubisho na maji. Na pia kuzuia magugu kubeba vimelea na wadudu wanaoweza kuathili mazao yako.

HATUA ZA UKUAJI WA MPAPAI.

  1. Kitalu - Wiki 1 - 6 -Hatua ya ukuwaji wa haraka baada ya kuamishiwa.
  2. Shamba - wiki 7 -16 -Maua na kuweka matunda.
  3. Wiki 17 - 21 -Kukua kwa matunda.
  4. Wiki 22 - 26 -Mavuno ya kwanza 
  5. Wiki 37 -kuendelea Week 37 ni miezi tisa au kumi sio kwa hiyo kilimo cha mapapai huchukua miezi 10 kupata mavuno 


GHARAMA 

  1. Kununua ekari moja inategemea na eneo ulipo na bei husika. 
  2. Kununua mbegu tsh 50,000-100,000.
  3. Kumwagilizia kila siku -upandaji -kuhamisha kutoka kwenye vitalu hadi kwenye shamba -machine ya kumwagilizia 1,500,000/- 
  4. Generator tsh lak 6 
  5. Mbolea tsh 100,000 kila mwez -na vibarua shambani -kulima kwa trekta 40,000 Gharama zote kama mil 3-4 hiv mpaka kuvuna.


MAVUNO NA FAIDA.
Kama umelima ekarI moja unaweza ukapata matunda 15- 35 kwa mvuno wa Kwanza tu twende kimahesabu EkarI ina miche 400-800 Tuseme tupate miche 600 kwa ekari, kila mche utoe matunda 20 chini kabisa 600×20=12,000.

Matunda Soko Kwa sasa unaweza ukauza kwa jumla jumla tsh 1500-3000 Tuuze kwa bei ya chini 1500 kwa kila papai 12000×1500=18,000,000/- Ukitoa Gharama za uendeshaji unaweza ukabaki na tsh 14,000,000 au toa 4,000,000 uweke kwenye dharura unaweza ukamake tsh 10 mil kwa ekar moja tu.
KANUNI ZA KILIMO BORA CHA PAPAI KANUNI ZA KILIMO BORA CHA PAPAI Reviewed by BENSON on December 23, 2017 Rating: 5

23 comments

  1. Safi sana hii napenda kilimo cha mapapai

    ReplyDelete
  2. hizo ni ndoto za mchana,kuna utofauti mkubwa sana kati ya maandiko na uhalisia...ila asante kwa mchango wako

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kabisa,hayo ni makadirio ya makaratasi, kwanza bei hiyo ya papai kwa bei ya jumla huwezipata sehemu zote, pigia hesabu ni 500 kwingine papai moja

      Delete
    2. Mahesabu ya kilimo bwana ukipigiwa kwenye makaratasi utajiona imeshakuwa tajiri, ingia shambani kwa vitendo utaomba poo

      Delete
  3. Zao zuri Kwa biashara na ukuaji Wake ni haraka ,changamoto soko

    ReplyDelete
    Replies
    1. kuhusu soko kuna viwanda vinapokea mapapai ila tatzo ni uzalishaji wetu ni mdogo,kwa mfano pale kiwanda cha mandenge kwa bakresa wanapokea lakini mpaka uwe na Taki kadhaaa za papai,pia unatakiwa uwe unazalisha mengi ili wakikupa mkataba wa kupeleka kila wiki usishinde.

      Delete
  4. je?? wakati mvua za masika zimeanza kunyesha,hakuna madhara yoyote ambayo yanaweza kujitokeaza kwa mmea wa mpapai hasa mvua zinapokuwa zinanyesha???

    ReplyDelete
  5. Hii sio uongo, Bali Mara nyingi mawazo ya kibiashara huwa na tabia ya ku- LET CHANGAMOTO =0. Kwa hiyo ili kupata hesabu kamili za makadirio ya faida itakulazimu kuingiza changamoto na extra cost kulingana na mazingira yako.

    Maana stori hii bado inaashumu shamba liko nyumbani(hakuna gharama za kwenda shamba na kupeleka mbolea, hakuna gharama za kuchimba mashimo na gharama za samadi,n.k

    ReplyDelete
  6. Mm nataka kujua ntapata wapi hiyo miche ya mipapai na garama yake ni Sh ngapi?

    ReplyDelete
  7. Asante sana kwa kutuelimisha
    Je sehemu yenye mchanga inaweza tumika kilimo hicho?

    ReplyDelete
  8. Hebu niconnect na hao wanunuzi/wateja wa mapapai pls

    ReplyDelete
  9. Hqpo kwenye bei bei ya papai unadanganya nakaa mbezi beachi bei ni 1500 nakuendelea kwahivyo bei ya jumla hawezi kuwa hivyo

    ReplyDelete
  10. Daaah hali itolewavyo kimaandishi inakuwa tofauti na uhalisia ila cha msingi wengi wetu hatufuati maelezo ya wataalamu ndio maana mazao huwa chanya pia tusisahau kumuomba Mungu ili kilimo kizae vizuri

    ReplyDelete
  11. naomnba maekezo wapi nitapata mbegu bora ya mapapai

    ReplyDelete
  12. Ni makala nzuri sana kikubwa ni kufanya na siyo maneno tu

    ReplyDelete
  13. Mkoani Rukwa Miche inaoteshwa

    ReplyDelete