IJUE AINA YA MIZINGA KUFUGIA NYUKI.

Image result for bee keeping
Mizinga ya kufugia nyuki inapaswa kuandaliwa mapema kabla ya msimu wa kukamata makundi ya nyuki haujafika.Mizinga inayopaswa kuandaliwa ni kama ifuatayo:-


1. Mzinga wa kibiashara
Huu ni mzinga wa kisasa unaotumika kwa wafugaji wa nyuki hasa wale wanaotaka kuvuna asali kwa wingi kwa ajili ya kuuza.Mzinga huu huweza kuzalisha asali kwa wingi kadri misimu ya uvunaji inavyoongezeka mwaka hadi mwaka.
Mzinga huu una sehemu kuu tatu kama zifuatazo:-



A.  Box la kuzalishia watoto wa nyuki
Ni box ambalo kwa kawaida huwa la kwanza kwa upande wa chini.box hili ndilo ambalo huwa na mlandfo wa nyuki kuingia na kutoka pindi wanapokwenda na kutoka kwenye utafutaji wa chakula.Box hili hutumika na malikia wa nyuki kwa kutagia mayai pamoja na kulelea watoto ambao husubiri kuanguliwa na kuwa nyuki kamili.



Pia box hili hutumika kwa ajili ya nyuki kuhifadhia chakula chao kwa ajili ya msimu wa kiangazi, msimu ambao huwa hauna maua yenye chakula cha nyuki cha kutosha,Hivyo mfugaji hapaswi kuvuna asali anayoikuta katika brood box, kwa kuvuna asali unayoikuta katika brood box husababisha kundi lako kuhama kwa kukosa chakula.



Kwa kawaida matumizi ya mzinga huu huanza kuvuna asali baada ya wastani wa misimu miwili mikubwa yaani sawa na miaka miwili.Na mara baada ya kipindi hicho kipita mfugaji huweza kuanza kuvuna kwa vipindi tofauti tofauti vya mwaka na kuendelea.



B. Kitenga malikia
Hiki ni kifaa kama nyavu ambacho huwekwa kati ya brood box na super box, wavu huu huweza kumzuia malikia asiweze kupanda katika super box kwa lengo la kutaga mayai.matundu ya waya huu ni madogo kulingana na umbile la nyuki watenda kazi peke yao.Hivyo malikia na madume ya nyuki hayawezi kupanda kuelekea kwenye super box.



C. Box la kuhifadhia asali
Hili ni box ambalo huwekwa juu mara tu baada ya queen excluder.Box hili huwa ni maalumu kwa nyuki watenda kazi kuweza kuhifadhi asali yao kwa wingi.Asali inayokuwa katika box hili haiwezi kuchanganyika na watoto wa nyuki wala chavua kutokana na kuwapo kwa queen excluder chini yake.Asali inayotoka katika Box hili huwa nzuri na safi kutokana na kutochanganyika na masega ambayo yalitumika kwa kuangulia watoto wa nyuki.



Uvinaji wa asali katika mzinga huu, mfugaji anapaswa kutoa frame zilizopo katika super box ambazo asali yake tayari imeiva.Mara baada ya kutoa frame hizo mfugaji anapaswa kukamua asali hiyo kwa kutumia mashine ya kisasa iitwayo  Honey Centrifuge Machine.Mashine hii huweza kufyonza asali yote iliyopo katika sega na kubakiza sega likiwa halina asali.



Mara baada ya hapo mfugaji anapaswa kurudisha sega hilo kwenye mzinga likiwa na frame yake ili nyuki aweze kujaza asali tena.Hii inamsaidia sana nyuki kumpunguzia kazi ya kujenga sega jipya la Sali kila baada ya mvuno wa asali na hivyo kuongeza uzalishaji wa asali mara dufu.Tofauti tu ya aina ya mzinga huu ni kwamba huwezi kupata zao la nta.



2. Mzinga wa viunzi
Huu ni mzinga wa teknolojia ya kati kutoka kwenye mizinga ya kienyeji na kuelekea mizinga ya kisasa.Mzinga huu uhifadhi wake wa asali hautofautiani sana na uhifadhi wa asali katika mizinga ya kienyeji, isipokuwa katika mzinga huu masega hupangwa kwa kufuata utaratibu wa viunzi vilivyowekwa.nyuki huweka sega moja katika kila kiunzi kimoja cha mzinga huu.



Mzinga huu pia haujagawanywa kwa kutenganisha sehemu za kuhifadhia asali na sehemu ya malikia kuangulia watoto.Hivyo asali itokayo katika mzinga huu huweza kuchanyanyika na watoto iwapo mfugaji hatakuwa makini katika uvunaji wa asali hiyo.



Uvunaji wa mzinga huu, mfugaji anapaswa kukata sega lote lenye asali pekee na kulihifadhi katika chombo kisafi kwa jili ya kukamua asali hiyo kwa kutumia mashine ya kusasa au kwa kutumia njia za kitamaduni.



IJUE AINA YA MIZINGA KUFUGIA NYUKI. IJUE AINA YA MIZINGA KUFUGIA NYUKI. Reviewed by BENSON on December 16, 2017 Rating: 5

1 comment