IJUE MBOLEA YA ASILI ITOKONAYO NA MAGUGU MAJI.
Hii ni
aina ya mbolea ya asili isiyokuwa na madhara yoyote kwa binadamu na wanyama.
Mbolea hii hutengenezwa kwa kuvundika mimea ya baharini au maotea ya majini.
Aina hii ya mbolea inafaa kutumika kwa kuchanganya na viua wadudu vyovyote
ambavyo ni asidi au basic kwani utendaji kazi wake hauwezi kupote endapo
itachanganywa.
Viambata
vya mbolea
Mbolea
hii ina vichocheo vya mimea ambavyo ni vya asili kama Auxins,
Cytokins na Gibberellins ambavyo hivi ni homoni za
mimea ya asili yenye uwezo mkubwa wa kufanya mazao yaweze kumea vizuri na
hatimaye kutoa mavuno mazuri Mbolea hii pia ina madini zaidi ya sabini ambayo
yana uwezo mkubwa wa kustawisha na kuimarisha mazao kwa kiwango cha juu.
Kazi za
mbolea hii
1.
Inaongeza uwezo wa mmea kuweza kufyonza madini na virutubisho mbali mbali
kutoka kwenye udongo na pia kutoa mizizi kwa haraka.
2. Mbolea
hii pia inaongeza uwezo wa mimea kujitengenezea chakula chake yenyewe.
3. Ina
uwezo wa kusaidia uhifadhi wa unyevu nyevu katika udongo kwa muda mrefu.
4.
Inafanya mmea uweze kuhimili hali ya ukame, ubaridi pamoja na magonjwa
mbalimbali.
5.
Inafanya mmea uweze kuota mapema kuongeza wingi wa mizizi na mimea kuwa na afya
6.
Inaongeza kiwango cha mavuno ya mazao yako.
7.
Inaongeza muda wa matunda au mazao kukaa muda mrefu baada ya mavuno kama
ikitumiwa siku kumi kabla ya kuvuna.
Mimea
ambayo inastahili mbolea hii
Mbolea
hii inaweza kutumika katika mimea au mazao mbalimbali kwa mfano matunda yoyote,
mboga za majani, mazao ya nafaka, dawa za mitishamba, maua, nyasi, pamba,
nyanya, hoho, bilinganya, vitunguu, nk.
Pamba
Unaweza
kutumia kuloweka mbegu zako kabla ya kupanda kwa kuchukua kiasi cha mililita 40
za bioplus na kuweka kwenye lita 20 za maji kisha kuloweka mbegu
zako kwa masaa 5 hadi 10 ndipo uzitoe tayari kwa kupandwa. Inashauriwa kutumia
kiwango cha mbolea cha mililita 60 hadi 90 kwa ekari moja. Wakati wa kutoa maua
unashariwa kutumia kiwango cha mililita 180 kwa hekari moja. Kwa mara moja,
changanya mililita 13 - 20 za mbolea kwenye lita 20 za maji na kisha nyunyizia
kwenye mazao.
Mpunga
Kwa
kuloweka mbegu, chukua mililita 60-90 za mbolea ya bioplus kisha
changanya kwenye lita ishirini za maji na weka mbegu zako kwenye maji masaa
manane mpaka kumi ndipo uzitoe tayari kwa kupandwa. Hiki kiwango unaweza
kubadili kulingana na lita za maji unazotumia hivyo unaweza kutafuta ni kiasi
gani cha dawa unachohitaji kuchanganya kwenye maji. Baada ya kuanza kutoa maua,
chukua mililita 13-20 kisha weka kwenye maji ya lita 20 na nyunyuzia kwenye
mazao. Hakikisha kuwa hekari moja hauzidishi kiasi cha mbolea chenye wingi wa
mililita 240 kwa ekari moja.
Mahindi
Kwa
kuloweka mbegu, chukua kiasi cha mililita 40 za bioplus na
changanya kwenye maji lita 20. Weka mbegu zako ndani ya mbolea kwa masaa 8-10.
Mahindi yakishatoa majani na maua, Chukua mililita 20 za mbolea kisha weka
kwenye maji lita 20 na nyunyuzia mahindi. Hakikisha huzidishi kiwango hiki, na
tumia mililita 720 za mbolea kwa ekari moja.
Mboga za
majani
Chukua
mililita 40 za mbolea kasha weka kwenye lita 20 za maji na nyunyuzia mboga.
Unashauriwa usizidishe 720 mls za mbolea kwa hekari moja na unaweza kunyunyuzia
mara tatu kwa kipindi chote cha zao kuwa shambani.
Matango,
tikiti na nyanya
Chukua
mililita 20 za mbolea kasha changanya na lita 20 za maji na nyuny-uzia kwenye
mazao yako. Unashauriwa usizidishe kiasi cha 720mls kwa kila ekari kila
unaponyunyuzia hii mbolea, na waweza kunyunyuzia hadi mara tatu mpaka kufikia
mazao yako kuvuna. Pia unaweza kuitumia mbolea hii kwa mazao mengine kama
matufaha, ndizi, maembe, soya nk.
Kwa
maelezo zaidi wasiliana na mtaalamu Bi. Josepher Philemon kwa simu
0713123995/0755 522018
IJUE MBOLEA YA ASILI ITOKONAYO NA MAGUGU MAJI.
Reviewed by BENSON
on
October 31, 2017
Rating:
Namna au jinsi yakutengeneza mboleahiyo amakuanda unafanyaje?
ReplyDelete