JIFUNZE KILIMO BORA CHA ALIZETI
Hali ya hewa na udongo.
Alizeti ni zao linalostahimili ukame pia kwenye sehemu za mvua za wastani pia huwezwa kulimwa kuanzia ukanda wa pwani hadi maeneo ya mwinuko. Kwa hapa tanzania alizeti hulimwa kwa wingi katika mkoa wa singida.
Unashauriwa kutayarisha shamba lako mapema kwa kukatua ardhi na kulainisha vizuri. Samadi yaweza kuchanganywa vizuri na udongo wakati wa kuandaa shamba.
Wakati sahihi wa upandaji alizeti.
Upandaji wa alizeti hutegemea sana hali ya hewa ya eneo husika.
Maeneo yenye mvua nyingi alizeti huanza kupandwa mwishoni mwa mwezi Januari mpaka katikati ya mwezi Februari.
Maeneo yenye mvua kidogo alizeti hupandwa mwezi Desemba hadi Januari.
Kiasi cha mbegu na namna ya kupanda alizeti.
- Kiasi cha kilo 3 – 4 za mbegu zinatosha kupanda eneo la ekari moja.
- Panda mbegu 3 – 4 katika kila shimo moja kwa nafasi ya sentimita 75 kutoka mstari hadi mstari na sentimita
- 30 kutoka shimo hadi shimo au sentimeta 75 kwa 40 au Sentimeta 90 kwa 30 kwa mbegu kubwa.
- Shimo la mbegu liwe na kina cha sentimita 2.5 – 5.
Wiki mbili baada ya kuota, punguza miche katika kila shimo na kubakiza
Mbolea zinazofaa kwa kilimo cha alizeti ni zile za kupandia na kukuzia hasa kwenye maeneo yasiyo na rutuba.
Wakati wa kupanda tumia nusu mfuko kwa ekari moja ya mbolea ya kupandia na mfuko mmoja kwa ekari moja ya mbolea ya kukuzia kwa kuigawa mbolea hiyo mara mbili. Nusu ya kwanza iwekwe wakati wa kupanda na nusu ya pili iwekwe wiki mbili baadaye. au Pandia mbolea ya TSP au DSP, au SSP na Kuzia kwa SA baada tu ya palizi ya Kwanza (wiki mbili hadi tatu baada ya mimea kuota)
Wakati wa kuweka mbolea angalia isigusane na mbegu au mche wa alizeti kwani huunguza.
Palizi.
Alizeti hukua taratibu katika wiki chache za mwanzo. Hivyo unashauriwa kupalilia mapema ili kupunguza hasara. Katika maeneo yaliyo na magugu machache, palizi moja tu inatosha. Vile vile maeneo yenye upepo mkali, wakati wa kupalilia inulia matuta ili kuzuia kuanguka.
Wanyama na wadudu wanaoathiri ukuaji wa alizeti.
1..NDEGE
Alizeti hushambuliwa sana na ndege ambao huweza kuteketeza hadi asilimia 50 ya mazao shambani.
Kuzuia
- - Usipande alizeti karibu na msitu/pori
- - Vuna mapema mazao yako mara baada ya kukomaa.
- - Panda alizeti kwa wingi katika shamba moja.
- - watishe ndege kwa mutumia sanamu, makopo.
2..Funza wa vitumba.
Funza huyu hutoboa mbegu changa kuanzia mara tu vitumba vya maua vikifunguka mpaka karibu na
kukomaa kwa mbegu.
Kuzuia:
- Tumia dawa yo yote ya kuulia wadudu inayopatikana katika maduka ya mifugo.
Alizeti hushambuliwa na magonjwa yakiwemo madoa ya majani, kutu, kuoza kwa mizizi, shina, kichwa na kushambuliwa na virusi.
Kuzuia:
- - Tumia kilimo cha mzunguko wa mazao
- - Panda mbegu safi zilizothibitishwa na wataalamu
- - Choma masalia ya msimu uliopita
- - tumia madawa yanayotumika kuulia wadudu waaribifu.
Uvunaji wa alizeti.
Unashauriwa kuvuna alizeti mara tu inapokomaa ili kupunguza hasara ya kushambuliwa na ndege. Alizeti iliyokomaa kichwa hubadilika rangi toka kijani kibichi na kuwa njano. Kata vichwa na kuvianika juani ilivikauke vizuri.
Piga piga vichwa ili kutoa mbegu za alizeti, kisha upepete na kuendelea kuzianika ili zikauke vizuri.
Utafiti unaonyesha kuwa mkulima anaweza kupata magunia kati ya 10 -12 kutoka katika ekari moja.
JIFUNZE KILIMO BORA CHA ALIZETI
Reviewed by Muungwana Blog
on
April 30, 2017
Rating:
No comments