FAHAMU KUHUSU UANDAJI NA UOTESHAJI WA MBEGU ZA MITIKI


Matayarisho:


  • Ganda la nje la mbengu ya mtiki ni gumu sana na lina sumu mbaya.Unatakiwa uloweke mbegu ya mitiki kwa masaa 72, na kila baada ya masaa 12 unatakiwa ubadilishe maji kwa kumwaga maji ya zamani na kuweka maji mapya.


  • Baada ya masaa 72 anika mbegu zako juani kwa masaa 12 (zianikike ktk bati).


  • Tengeneza kitalu, weka mbolea ya wanyama au mboji, kisha panda mbegu zako kwenye kitalu.


  • Mwangilia maji kila siku asubuhi na jioni, mbegu zitaanza kuota baada ya siku 10 hadi 20.


  • Miche ikifikia urefu wa futi moja, unaweza sasa kuiotesha kwenye shamba lako ulilotayarisha kwa ajili ya kuotesha miti.


  • Kabla ya kung'oa miche hakikisha unamwaga maji mengi, ili mizizi isikatike sana, kisha chukua kisu chenye makali ya kutosha na kata ncha ya juu ya mti na ondoa majani, hii inasaidia mti kuchipuka upya hasa eneo ambalo halina maji mengi.


  • Otesha miti futi 6x6 mitiki inaposongamana, hurefuka haraka ikikimbilia jua angani, hivyo kwa vipimo hivyo miti yako itakuwa mirefu sana na iliyonyooka, baadaye unaweza kuipunguza na kuuza fito za kujengea.


  • Ili upate mbao bora hakikisha unaondoa matawi yanayochipuka pembeni hadi mti ufike zaidi ya futi 10 kwani ndiyo yanafanya mbao kuwa na mabaka (vidonda).
FAHAMU KUHUSU UANDAJI NA UOTESHAJI WA MBEGU ZA MITIKI FAHAMU KUHUSU UANDAJI NA UOTESHAJI WA MBEGU ZA MITIKI Reviewed by BENSON on June 17, 2018 Rating: 5

No comments