YAJUE MAGONJWA MAKUU YA KUKU, DALILI, NA TIBA ZAKE

Tokeo la picha la magonjwa ya kuku

Kila ugonjwa huwa na dalili zake kuu ambazo hutofautisha na magomjwa mengine, ingawa zipo zile za kufanana mfano kutokula vizuri, kushusha mabawa, kuzubaa/kusinzia na joto kuwa juu

No 1: NEWCASTLE /KIDERI / MDONDO
Dalili kuu: Kupindia shingo juu au chini, mwendo wa kuzungukazunguka, kutembea mwendo wa kurudi nyuma huku kichwa kikiwa kimepindia chini au juu. Dalili isiyo kuu ni mharo rangi ya kijani
Tiba:Ugonjwa huu husababishwa na virusi kwa hiyo hauna tiba. kinachotibika ni hizo dalili tu ila ugonjwa hubaki kwenye damu hivyo tumia Trimazine 30% na mult vitamin.

No 2: GUMBORO / INFECTIOUS BURSAL DISEASE.
Dalili kuu:Kuharisha rangi nyeupe kama chokaa. Ukimpasua baada ya kufa kunakuwa na kama matone ya damu kifuani na kwenye firigisi sehemu ya mbele
Tiba:Ugonjwa huu husababishwa na virusi kwa hiyo hauna tiba.

NO 3: MAREK'S DESEASE/ MAHEPE
Dalili kuu:kuparalyse /kukakamaa and kwa miguu na mabawa, Hapa mguu mmoja mara nyingi huwa mbele na mwingine nyuma, kuvimba kwa kihifadhia chakula (crop), kwa kuku wa mayai huathiriwa wakiwa wadogo ila madhara hutokea wakifikisha miezi 5 wakianza kutaga.
Tiba:Ugonjwa huu husababishwa na virusi kwa hiyo hauna tiba.

NO 4: NDUI YA KUKU / FOWL POX.
Dalili kuu:Vipele sehemu zisizokuwa na manyoya kama vile vilemba vya kichwani (comb na wattle), puani na miguuni.
Tiba:Ugonjwa huu husababishwa na virusi kwa hiyo hauna tiba., kupunguza madhara waoshe kwa maji ya uvugu vugu yenye chumvi ya mawe hadi Vipele viishe au vipake mafuta na mpe antibiotic kama Otc 20%.

No 5 MAFUA MAKALI/ INFECTIOUS CORYZA
Dalili kuu:Chafya, kusinzia, kuvimba sehemu za  uso, kichwa  na macho, ute mzito mweupe jichoni hupelekea jicho kuziba, udenda puani na mdomoni.
Tiba: Fluban, au  Tylodox au OTC 20 %, Tylosan, changanya na mult vitamin.

No 6: FOWL TYPHOID/ HOMA YA MATUMBO
Dalili Kuu:Mharo rangi ya njano.
Tiba: Esb3, Trimazine 30%, Tylodox.

NO 7 COCCIDIOSIS/ MHARO DAMU.
_Dalili kuu: Kinyesi/mharo rangi ya ugoro mwanzo na unavyoendelea kinakuwa rangi ya damu.
Tiba: Amprolium 20%,Esb3, Trimazine 30%, Vitacox, na Agracox.

NO 8: FOWL CHOLERA/ KIPINDUPINDU CHA KUKU.
Dalili kuu: kinyesi mharo wa kijani.
Tiba: Trimazine 30 % au Esb3.

NO 9 MAGONJWA MATATIZO YANAYOTOKAN NA LISHE DUNI
_Kuvimba macho, miguu kukosa nguvu na kashindwa kusimama au kutembea, kutaga mayai tepetepe, kula mayai, kudonoana.
Tiba: Chakula kiwe na mchanganyiko mzuri wa mult vitamin na protein, kwa wanaodonoana kata au choma midomo yao na uwape mboga za majani ukiwa umezining'iniza juu kidogo.


Kama utawapa kuku wako wa wanaotaga mayai dawa zenye sulphur ndani watapunguza kutaga mayai, kwa hiyo kama utaweza kupata dawa ambayo haina sulphur ndani yake itakuwa ni vizuri zaidi
YAJUE MAGONJWA MAKUU YA KUKU, DALILI, NA TIBA ZAKE YAJUE MAGONJWA MAKUU YA KUKU, DALILI, NA TIBA ZAKE Reviewed by BENSON on October 17, 2017 Rating: 5

No comments