ZIJUE FAIDA ZA KULIMA MAPAPAI

Related image




Hili ni aina ya zao la matunda linalopatikana katika familia ya caricaceae na linajulikana kwa jina la kisayansi carica papaya

Papai ni moja ya matunda ambayo huchukua muda mfupi hadi kufikia mavuno. Huchukua muda wa miezi 8-9 kufikia mavuno. 
Matunda katika mpapai utokeza katika kila jani na mpapai kwa wiki moja unauwezo wa kutengeneza majani mawili na kwa makadilio mpapai huanza kutengeneza maua katika jani la
32 hii ikimaanisha ni baada ya wiki nne.

FAIDA KIUCHUMI
Hekari moja inauwezo wa kuwa na mipapai 1000-2500. Mavuno ya mapapai kwa miezi 8 - 9 kwa mavuno ya kwanza ni tani 40 - 60 ikiwa kila mpapai unaweka matunda 40 hadi 50 kwa miezi 8 - 9. Baada ya mavuno ya kwanza, mavuno ya mapapai hayana msimu hivyo yataendelea ndani ya miaka mitano katika uangalizi mzuri wa mipapai yako hadi kufikia kipindi ambacho mpapai wako utapokufa..


JINSI YA KUJUA FAIDA
 Kwa matunda 40 - miti 1000 jumla ya matunda 40,000 yatavunwa
Bei ya papai Tsh. 500 kwa papai
 500 x 40,000 = 20,000,000/=
 Hivyo kwa kila mwezi ni tsh. 2,500,000/= kwa mipapai ya miezi 8 kufikia mavuno.

Mahitaji
Mahitaji ya mipapai kwa mwezi hayazidi 500,000/-= hivyo unauhakika wa kupata faida ya 2,000,000/= kwa mwezi kutokana na zao la mapapai.




FAIDA ZA PAPAI KIAFYA.

Kama matunda mengine, papai  nalo lina faida zakekiafya na pia huweza kutumika kama dawa kwa baadhi ya matatzo ya kiafya,  kama una tatizo la choo kubwa ni nzuri. Halafu jambo jinginge papai ni kilainisho kizuri sana cha chama hasa nyama ya ngómbe. Toa hizo mbege weka kwenye chombo, pondaponda papai na uchanganya na hizo mbegu koroga taratibu katakata nyama vipande vidogovodogo weka humu kwenye mpondo na subiri masaa kadhaa. Hakika utaifaidi nyama yako mno itakuwa lainiiii.


 Muhimu: Maelezo hayo ni kwa ufupi na kwa bei ya kawaida sana na bei ya papai lenye kilo nzuri huzidi hapo. Pia mavuno huweza zidi hapo kwa maana hiyo faida huenda mbali zaidi ya hapo. 
ZIJUE FAIDA ZA KULIMA MAPAPAI ZIJUE FAIDA ZA KULIMA MAPAPAI Reviewed by BENSON on May 06, 2018 Rating: 5

No comments