UMUHIMU WA KUFAHAMU VYANZO VYA MAGONJWA YA MIFUGO
Magonjwa mengi ya mifugo husababishwa na vyanzo
kutoka nje ya mwili wa mnyama mfano; mazingira machafu anayoishi mnyama, vitu
vinavyopelekea vidonda (vitu vyenye ncha kali) ambavyo husababisha vidonda na
baadaye vimelea vinaweza kukaa.
Pia mnyama anaweza kupata ugonjwa kutokana na hali za ndani ya mwili
kama upungufu wa lishe, mfano; madini na magonjwa ya kurithi.
Wadudu waenezi wa magonjwa ni kama vile;
Vimelea (bakteria)
Mfano
wa magonjwa yanayosababishwa na vimelea ni kama vile chambavu, black
quarter, kimeta, kifua kikuu, brucellosis,
ugonjwa wa kiwele, na ng’ombe dume kuvimba mapumbu.
Virusi (virus)
Mfano wa magonjwa yanayosababishwa na virusi ni
kichaa cha mbwa (rabies), ugonjwa wa midomo na miguu
(foot and mouth disease) nansotoka (rinderpest).
Protozoa
Magonjwa yanayosababishwa na protozoa ni kama
ndigana baridi, ndigana kali, ndigana mkojo damu na ndigama maji moyo na
nagana.
Lishe duni
Upungufu wa viinilishe katika chakula cha
mifugo husababisha madhara katika mwili kama ifuatavyo;
• Husababisha majike kutopata joto mapema
• Ndama kuzaliwa na viungo visivyokomaa
• Upungufu wa uzalishaji wa maziwa
• Kiwango cha uzalishaji kushuka.
Vidonda/michubuko
Kupitia vidonda au michubuko, wadudu
wasababishao magonjwa huingia mwilini mwa mnyama na kuleta madhara.
Magonjwa ya kurithi
Kama mmoja wa wazazi ana magonjwa au ugonjwa wa
kurithi basi kuna uwezekano mkubwa wa mmoja wa ndama watakaozaliwa kurithi
ugonjwa huo.
Utunzaji bora wa afya ya mifugo
Uogeshaji
Mifugo waogeshwe mara kwa mara ili kuepukana na
magonjwa yaenezwayo na kupe pamoja na ndorobo. Uogeshaji unaweza kufanyika kwa
kutumia pampu za mgongoni au kwa kuwatumbukiza katika josho lililotiwa dawa ya
kuogesha.
Kuwapa dawa za minyoo
Mifugo wapatiwe dawa za minyoo mara kwa mara
ili kuhakikisha ukuaji wao na utoaji wa maziwa uendelee vizuri. Mifugo
wapewe dawa za minyoo kila baada ya miezi mitatu.
Kuhasi
Ndama dume wasiohitajika kwa ajili ya kuzalisha
baadaye, wahasiwe kwa njia ya upasuaji au kwa kutumia koleo au badizo iwapo
ndama ni wakubwa.
Kuwapa ndama alama za utambulisho
Ndama wapewe namba au alama za utambulisho mara
wafikiapo miezi 6 tangu kuzaliwa na utambulisho huu unaweza kuwa wa chuma au wa
plastiki chenye namba kwenye sikio.
Kuondoa vishina au vichomozo vya pembe
Ndama waondolewe pembe katika mwezi wa kwanza
tangu kuzaliwa kabla vishina havijakomaa na kusababisha kushindwa kutoka kwa
miezi ya mbeleni. Tumia chuma cha moto kutoa vichomozo vyote vya pembe na hii
husaidia ndama kukua katika mwonekano mzuri na kutokuwa na pembe zinazoweza
kuumiza wenzake pindi ziwapo kubwa.
Kuondoa kwato
Kwato za ndama ziondolewe miezi mitatu ya
mwanzo, ili kusaidia kupunguza kuondokana na magonjwa ambukizi ambayo
husababishwa na kukatika kwa kwato zikiwa kubwa pindi awapo malishoni au akiwa
katika banda lenye sakafu ya saruji.
UMUHIMU WA KUFAHAMU VYANZO VYA MAGONJWA YA MIFUGO
Reviewed by BENSON
on
October 11, 2017
Rating:
nimependa mwongozo wenu
ReplyDeletepia ninaitaji huduma yenu 0786092073