BANDA BORA LA KUKU NI LAZIMA LIWE NA HIVI

Zifuatazo ni sehem za banda bora la kuku kulingana na aina ya
kuku:-
1. Sehem
za kutagia (kama ni kuku wa mayai au wa kienyeji).
Katika banda bora la kuku
wanaotarajiwa kutaga inapaswa kuwepo na sehem za kutagia zijulikanazo kwa jina
la viota. Viota vinaweza kutengenezwa kwa mtindo wa kuku mmoja mmoja au
ushirika.
2. Sehem
ya kutembelea.
Ni ukumbi mkubwa kulingana na
idadi ya kuku, ambao ndani yake kunakuwa na vyombo vya maji na chakula, pamoja
na kuku wenyewe.
3. Sakafu
Zipo aina mbalimbali za sakafu kama
ifuatavyo:-
a) Sakafu
ya saruji
Ni vema zaidi ukajenga sakafu ya
saruji kisha ukaweka maranda juu yake ili kuzuia ubaridi
unaotoka sakafuni, na vilevile kupata wepesi wakati wa kufanya usafi.
b) Sakafu ya udongo au mawe
Jaza udongo wa mfinyanzi au mawe kisha siliba
vizuri acha pakauke mwisho weka Maranda kwa wingi.
c) Sakafu
ya chaga
Banda hujengwa
kisha huwekwa chaga umbali wa futi mbili kutoka chini, chaga inaweza
ikawa ya banzi,
"chicken wire" au fito ili kuruhusu kinyesi cha kuku kudondoka
choini.
4. Ukuta
Unaweza kujenga ukuta kwa kutumia
nguzo, pamoja na mabanzi au fito kisha kuzibwa vizuri na kuacha sehemu kubwa
kwa ajili ya madirisha. Pia unaweza kutumia tofali za kuchoma, saruji au tofali
za udongo kwa kujengea na kuacha sehem kubwa kwa ajili ya madirisha.
5. Paa
Vifaa vya kuezekea vinaweza kuwa ni
vigae, nyasi, makuti au bati.
Kwa heshima na taadhima napenda
kutumia fursa hii kukusalimia wewe mdau wa mifugo na ambaye si mdau wa
mifugo lakini unapenda kufuatilia mafunzo yetu.
Pia napenda kuwakaribisha katika
darasa letu la ufugaji, tutakuwa tunawaletea
mada mbalimbali zinazohusu masuala
mazima ya ufugaji.
Lengo kuu la darasa letu la ufugaji
ni kumfanya mfugaji afuge kwa......
kufuata kanuni za ufugaji
bora ili ufugaji wake uwe ni wenye tija na kumpatia faida kwa ujumla.
Malengo mengine kama yafuatayo:
- Kumfanya mfugaji aboreshe maisha yake kupitia
ufugaji mifugo yake
- Kuboresha afya za watumia mazao ya mifugo kama
vile, Nyama, Mayai, na Maziwa kwa kuwa watatumia mazao ya mifugo kwa
kanuni bora za ufugaji.
- Kuongeza upatikanaji wa ajira kwa
vijana, watu wazima na wazee kwa ujumla kupitia ufugaji mdogo wa kati na
mkubwa.
- kuongeza matumizi sahihi ya nguvu kazi
na rasilimali watu kupitia ufugaji.
Hivyo basi ukiwa kama mdau wa mifugo
au si mdau lakini unapenda kufatilia darasa letu, tunakukaribisha tena na
tena katika kufatilia mfululizo wa mada mbalimbali katika darasa letu
tunasema karibu sana
BANDA BORA LA KUKU NI LAZIMA LIWE NA HIVI
Reviewed by BENSON
on
January 24, 2018
Rating:
No comments